Friday 15 December 2017

KIMATAIFA LEO: ZIMBABWE Wakulima Wazungu nchini Zimbabwe, warudishiwa Mashamba yao. Ni utekelezaji wa serikali mpya.

Serikali mpya ya Zimbabwe chini ya Rais Emmerson Mnangagwa, kupitia kwa Waziri wake wa Kilimo Perence Shiri imetoa amri kurudishwa mashamba yaliyokuwa yakimilikiwa na wakulima Wazungu, ambao walinyang’anywa wakati wa utawala wa Robert Mugabe na kupewa raia wa Zimbabwe
“Wote ambao wamepewa mashamba kinyume cha sheria wanapaswa kuyarudisha haraka iwezekanavyo,” – Perence Shiri,.
Waziri Shiri amesema kuwa wale ambao wana vibali rasmi wataruhusiwa kuendelea kulima katika mashamba hayo ili kuhakikisha uzalishaji. Shiri amesema hatua hiyo inalenga kukuza kilimo kwa ajili ya uchumi wa nchi hiyo ambao unaendelea kudorora kila kukicha.

“Ikiwa tunataka kufanikisha malengo yaliyowekwa na serikali ni lazima tutumie kilimo kama nguzo ya uchumi, lazima tuhakikishe utaratibu mzuri wa kilimo,” – Perence Shiri

0 comments: