Ikiwa zimepita siku 16 tangu kuuawa kwa
askari 14 wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) waliokuwa kwenye
oparesheni ya ulinzi wa amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo,
Waziri wa Ulinzi wa Tanzania Husssein Mwinyi amewatembelea wanajeshi wa Tanzania waliopo nchini humo.
Mwinyi
alifika nchini humo December 22, 2017 ambapo alipowatembelea Wanajeshi
wa Tanzania wanaoshiriki katika kikosi cha kimataifa cha kulinda amani
mashariki ya Congo, na kuwatembelea wanajeshi waliojeruhiwa wakati wa
shambulizi la December 7, 2017.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Beni, Mwinyi
ametoa wito wa kudumisha ushirikiano kati ya pande zote zinazoshiriki
katika kuleta amani Mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).
Wanajeshi 14 wa Tanzania wa kikosi
maalum cha nchi za Kusini mwa Afrika SADC waliuawa na wengine 44
kujeruhiwa wakati wa majibizano ya risasi na waasi wasiojulikana katika
kambi yao huko Semulik, karibu na mji wa Beni.
0 comments: