Sunday 24 December 2017

Thamani Dau la Simon Msuva lapanda kufikia zaidi ya Million 300.


Klabu ya Difaa El Jadida ya Morocco ilimnunua winga Simon Msuva kutoka Yanga Julai mwaka huu kwa dau la dola 100,000, lakini sasa thamani ya mchezaji huyo imepanda hadi pauni 113,000 sawa na dola 151,054.

Hiyo ina maana kwamba, kwa fedha ya Tanzania, Msuva aliyenunuliwa kwa dola 100,000 ambazo ni sawa na Sh milioni 222.4, sasa thamani yake ilipofika dola 151,054 ni sawa na Sh milioni 335.9.

Kwa mujibu wa takwimu za soka zinazofuatilia maendeleo ya mchezaji na kumpangia thamani, Msuva amepanda bei kwa takwimu ambazo zimechukuliwa hadi Oktoba 24, mwaka huu.

Hadi sasa akiichezea klabu yake hiyo ya Morocco, Msuva amefunga mabao matano katika Ligi ya Morocco huku akifunga mengine tisa katika mechi nyingine zisizo za ligi, jumla anayo 14.

Tangu amejiunga na klabu hiyo ya Difaa, Msuva amekuwa na wastani mzuri wa ufungaji kiasi cha kuwa miongoni mwa wachezaji tegemeo katika kikosi chao licha ya ugeni wake.


Mkataba wa Msuva na Difaa unafikia tamati Juni 30, 2020, lakini kutokana na maendeleo yake kuwa mazuri, kuna uwezekano wa winga huyo kuondoka klabuni hapo kabla ya kumaliza mkataba huo.

0 comments: