Ujenzi wa barabara
za awamu ya kwanza katika halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni jijini
Dar es salaam kupitia Ufadhili wa Mradi wa Benki ya Dunia DMDP
umekamilika kwa asilimia 80 huku kazi iliyobaki ikiwa ni ujenzi wa
mitaro ya kupitisha maji ya mvua,Uwekaji taa za barabarani pamoja na
njia za watembea kwa Miguu….
Akizungumza na Chanelten wakati wa Ukaguzi wa barabara hizo
zinazounganisha Tanesco kuelekea Soko la Samaki Msasani, barabara ya
viwandani eneo la Mwenge pamoja na barabara za Makumbusho, Mratibu wa
Usimamizi wa mradi huo katika manispaa ya kinondoni Mkelewe Masalu
Tungaraza amesema Mkandarasi aliyepewa kazi hiyo anatarajia kuIkamilisha
Januari mwakani.
Kuhusu awamu ya pili ya Ujenzi wa barabara za Tandale,Maji Vhumvi
-Kisukulu pamoja upanuzi na uwekaji kingo katika mto ng’ombe ili
kupunguza athari za Mafuriko katika makazi ya wananchi amesema tayari
Mkandarasi ameshapatikana na kazi imeanza,huku pia tathmini na malipo
kwa wananchi ambao sehemu za nyumba zao zitavunjwa wanaendelea kulipwa
fidia.
Mstahiki Meya wa Kinondoni Benjamini Sitta akizungumzia Umuhimu wa
Miradi hiyo amesema itasaidia kupunguza foleni kwa wakazi wa msasani na
maeneo yote ya makumbusho,lakini pia kupungua mafuriko ambayo imekuwa
ikiwaathiri wakazi wa maeneo hayo pamoja na kuongeza thamani makazi yao.
0 comments: