Kocha Shedrack Nsajigwa waYanga ameshindwa kuvunja mwiko wa kuifunga Mbao FC uwanja wa CCM Kirumba Mwanza
Yanga leo imejikutaikiangukiapuaMjini Mwanzabaadayakupokeakipigo cha mabao 2-0,kutoka kwawenyeji wao Mbao FC, huo ukiwani mchezo waLigi Kuu ya Tanzania Bara mzungukowa 12 ambao umepigwa uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.
Kipigo hicho cha leo kimeishuka Yanga kwenye msimamo kutoka nafasi ya tatu ilipokuwahadi nafasi ya nne na kuipisha Singida United kwenye nafasi hiyo huku Simba na Azam zikiendelea kujinafasi kwenye nafasi mbili za juu.
anga ambayo ilicheza bila nyota wake watano wa kikosi cha kwanza ambao wana matatizo mbali mbali wengine wakiwani majeruhi nawengine matatizo yakifamilia.
Wachezaji Habibu Haji na Boniface Maganga, ndio walipeleka kilio Jangwani na kufanya timu hiyo kuendelea kuwana wakati mbaya inapocheza kwenye uwanja wa CCM Kirumba baada yamsimu uliopita pia kupoteza mechi zote mbili dhidi ya Mbao FC.
Katika kipindi cha kwanza timu zote zilizcheza kwa nguvu na kushambuliana kwa kasi lakini washambuliaji wa timu zote mbili walishindwa kuzitumiavyema nafasi walizozipata na kufanya matokeo kuwa sare katika dakika 45 za kipindi cha kwanza.
Kipindi cha pili ndipo mambo yalipoanza kubadilika kwa vijana waYanga kushindwa kuhimili kasi ya Mbao FC, na kujikuta wakipachikwa bao la kwanza dakika ya 53 mfungaji akiwa Haji ambaye alifanya kazi nzuri baada ya kupokea pasi kutoka upande wa kushoto.
Bao hilo lilionekana kuwazindua Yanga nakufanya mashablizi mengi kwenye lango la Mbao lakini ulinzi wa kocha Ettienne Ndayiragije ulikuwa makini na kuondosha hatari zote langoni mwao.
Wakati Yanga wanapambana kusawazisha bao hilo walijikuta wakipachikwa bao la pili dakika ya 68, baada yamabeki wake kufanya uzembe ambao ulimfanya Boniface Maganga kuifungia timu yake bao hilo lililoipa ushindi wa pili msimu huu wakiwanyumbani.
0 comments: