Ikiwa
zimebaki siku sita tu kabla ya kuumaliza mwaka 2017 na kuingia 2018,
staa wa Bongofleva Barnaba Classic ametangaza kuwaaga mashabiki wake kwa
mwaka huu na atakuwa kimya kimziki kwa muda.
Mkali
huyo wa sauti na uandishi kwenye kiwanda cha mziki Bongo, ameweka wazi
kuwa ukimya wake utaanzia kwenye mitandao ya kijamii ikiwa ni sehemu ya
kujiandaa na kujipanga namna ya kuuanza kwa kishindo mwaka 2018.
“Nikiwa
najitoa kwenye mitandao ya kijamii kidogo, ningependa kuwatakia
mashabiki, marafiki na familia yangu Heri ya Christmas na Mwaka Mpya”, amefunguka Barnaba kupitia ukurasa wake wa Instagram.
Pamoja
na kujitoa kwake nyota huyo anayetemba na ngoma yake ya Mapenzi Jeneza
ameongeza kuwa anajiweka vizuri kuanzia mwonekano mpaka sound ya hit
zake zijazo.
“Ninapumzika
kidogo ili kuweka mipango yangu vizuri kwaajili ya mwaka 2018.
Nitawaletea Barnaba mpya mwenye kila jipya kimuziki na hata Sound” ameongeza.
0 comments: