Monday 18 December 2017

MICHEZO: Antoine Griezmann: Nyota wa Atletico Madrid aomba radhi baada ya kujifanya mweusi.

Mshambuliaji nyota wa Atletico Madrid na Ufaransa Antoine Griezmann ameomba radhi baada yake kushutumiwa vikali kwa kujipaka rangi nyeusi kama sehemu ya utani wa kubadilisha sura.
Alikuwa awali amewaambia wafuasi wake kwenye Twitter watulie kabla ya kulazimika kuchukua hatua hiyo.
Griezmann alikuwa amepakia kwenye Twitter picha yake akiwa amevalia kama mchezaji mweusi wa mpira wa kikapu.
Baadaye aliifuta picha hiyo, sawa na ujumbe wa pili aliokuwa ameuandika uliosema: "Tulieni nyote. Mimi ni shabiki wa Harlem Globetrotters na natoa heshima kwao."  (BBC SWAHILI)

0 comments: