Shirika la anga za juu la Marekani maarufu kama NASA siku za hivi
karibuni limegundua nyota ambayo inazungukwa na sayari nane, sawa na
mfumo wetu wa jua ambao una sayari nane.
Inaelezwa kuwa hiyo ndiyo idadi ya juu zaidi ya sayari kugunduiwa
zikiizunguka nyota nje ya mfumo wetu wa sayari. Nyota hiyo iliyopewa
jina Kepler-90, ina joto kiasi na ni kubwa kidogo kulishinda Jua.
Hapo awali, wataalamu wa anga za juu waligundua uwepo wa sayari saba
pekee zilizokuwa zinaizunguka lakini hivi karibuni wanasayansi wa Nasa
wamegundua uwepo wa sayari nyingine ndogo iliyojaa mawe ambayo ndiyo
inakamilisha idadi ya sayari hizo nane.
0 comments: