Ramposa ambaye alikuwa makamu wa rais wa chama hicho aliweza
kumshinda mpinzani wake Nkosazana Dlamini-Zuma, ambaye ni waziri wa
zamani na alikuwa mke wa rais Zuma kwa kura 2440 kwa 2161.
Kwa sasa Ramaphosa ameoneka kuwepo kwenye nafasi kubwa ya kuwa rais katika uchaguzi wa mwaka 2019.
Hata hivyo Cyril Ramposa amekuwa kiongozi wakati ambao Afrika kusini
inakabiliwa na changamoto nyingi ambazo zinafanya mambo hayendi sawa
katika taifa hilo lenye uchumi mkubwa barani Afrika .
Cyril Ramaphosa ni mtu wa aina gani?
Cyril
Ramposa alizaliwa tarehe 17 mwezi novemba mwaka 1952 mjini Soweto, ndio
mwanasiasa tajiri zaidi Afrika Kusini ,utajiri wake unakisiwa kuwa ni
dola milioni 450.Tangu ujana wake Ramposa alikuwa na ndoto ya kuwa
mwanasiasa shupavu na hiyo ndio ilimfanya kujiunga na uongozi wa chama
cha wafanyakazi, (BBC SWAHILI)
0 comments: