Kichapo cha Barcelona kwa Real Madrid na Record za Kibabe El Classico
Lionel Messi alifunga bao lililomfanya kufikisha mabao 25 katika El Clasico na hilo likiwa bao lake la 50 mwaka huu, Messi anakuwa amefunga mabao 50 kwa miaka 6 kuanzia 2010 akiwa ameacha 2013 tu.
Mchezo huu uliisha kwa sare ya bila kufungana katika kipindi cha kwanza na hii ikiwa mara ya kwanza kwa Barca kushindwa kufunga bao la katika kipindi cha kwanza Santiago Bernabeu tangu April 2011 katika La Liga.
Goli la kwanza la Barcelona lilifungwa na Luis Suarez likiwa ni bao lake la 5 katika El Clasico 7 alizocheza na huku Real Madrid wakishindwa kuweka clean sheet katika michezo ya El Clasico 7 iliyopita.
Lioneil Messi alimpoteza Cristiano Ronaldo hii leo kwani ukiachana na bao alilofunga lakini alikamilisha pasi 50/57,akitengeneza chance 9 na mashuti 3 on target, huku CR7 akikamilisha pasi 22/27,akitengeneza chance 1 na shuti 1 on target.
Bao la 3 la Barcelona lilifungwa na Alex Vidal dakika ya mwisho na kuifanya Barcelona kwa mara ya kwanza katika historia kushinda michezo 3 mfululizo ya El Clasico ugenini na hii ikiwa mechi ya 88.
Kwa mabao 2 ya leo yanaifanya Barcelona kumaliza mwaka na mabao 120 huku 39 wakifunga katika La Liga pekee na hii inawafanya kuwa timu inayoenda kumaliza mwaka na mabao mengi zaidi wakifuatiwa na PSG (103).
0 comments: