Saturday, 23 December 2017

IGP Sirro Atoa ONYO Zito kwa Waliojipanga Kufanya Uhalifu Msimu Huu wa Sikukuu

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Simon Sirro amefunguka na kuwataka watu wanaofikiria kutaka uharifu waache mara moja kwani wasipofanya hivyo wanaweza kujikuta wameishia gerezani au kukatishwa uhai wao na wakashindwa kusherehekea sikukuu.

Simon Sirro ametoa kauli hiyo mkoani Lindi, alipokuwa anazungumza na waandishi wa vyombo mbalimbali vya Habari.

Kamanda Sirro amesema mtu yeyote anayefikiria kufanya vurugu au vitendo vya uhalifu wa namna mbalimbali,ikiwemo wa kutumia siraha ni vema akaacha, vinginevyo anaweza akaishia gerezani au kupoteza maisha kabla ya hata hajashehelekea sikukuu hizo.

"Nasema tumejipanga vyema karibu timu zetu zote, zikiwemo za upelelezi, za kiinterijensia na timu zetu za operesheni nazo zimejipanga kwa ajili ya doria zikiwemo za helkopta, majini kila mahali kuhakikisha watanzania wanaishi kwa amani na utulivu ndani ya Taifa lao" Alisema Sirro.

Aidha Sirro alisema kuwepo kwa amani na utulivu kutawafanya wananchi mbalimbali, wakiwemo wafanyabiashara kutekeleza majukumu yao vizuri katika kujiletea maendeleo ndani ya nchi yao.

Mbali na hilo IGP Sirro, ameonya kwa kusema wale wanaofikiria kutumia silaha waachane na mpango huo  mara moja , kwa kuwa ni vigumu kumkamata mtu aliye na silaha na hivyo kitakachotokea ni ama mmojawapo kukatishwa uhai wake, huku akiwataka waalifu kujiuliza mara mbili kabla ya kuchukuwa silaha kwa lengo la kufanya uhalifu.

0 comments: