Wednesday 27 December 2017

Tuzo ya Mchezaji Bora aliyowahi Kupewa SAMATTA Yafutwa

Kama unaikumbuka tuzo ya mchezaji bora wa ndani wa Afrika ambayo Mbwana Samatta alishinda usiku wa January 7, 2017 haitakuwepo kwa mwaka huu 2017 kwa mara ya kwanza tangu ilipoanza kutolewa mwaka 1992.
Sababu ya msingi ambayo imetolewa na shirikisho la soka barani Afrika ni kwamba, waliopewa jukumu la kuchagua mchezaji bora wa kipengele hicho wote wamekosa sifa na walichaguliwa kimakosa kuwepo katika jopo hilo.
Kwa mujibu wa CAF tuzo hiyo huenda ikarudi endapo watapatikana watu sahihi watakaounda jopo ambalo kazi yake ni kuteua majina ambayo yatawania tuzo hiyo.
Kwa maana hiyo, kwa sasa wachezaji wa ndani watapambanishwa na wachezaji wanaocheza nje ya Afrika kuwania tuzo ya mchezaji bora hadi hapo itakapotangazwa vinginevyo.

0 comments: