Sunday, 24 December 2017

Ndege kubwa zaidi inayoweza kutua kwenye maji yafanya safari ya kwanza

Ndege mpya kubwa zaidi duniani inayoweza kutua na kupaa kutoka kwa maji ya china ya AG600, imefanya safari yake ya kwanza ya jumla ya saa moja.
Ndege hiyo ambayo ni kubwa kuweza kukaribiana na ndege ya Boeng ya 747 na yenye injini 4, ilipaa kutoka uwanja wa ndege wa Zhuhai katika mkoa ulio kusini wa Guangdong.
Ndege hiyo inaweza kubeba watu 50 na kusalia hewani kwa saa 12.
Ina mitambo ya kuzima moto na inaweza kufanya shughuli na uokoaji baharini na pia inaweza kutumwa kwenda eneo linalozozaniwa kusini mwa habari ya China.
Vyombo vya habari nchini China viliitaja ndege hiyo kama mlinzi wa bahari na visiwa.
Kupaa kwa ndege hiyo kulitangazwa moja kwa moja katika runinga ya taifa na ililakiwa na umati wa watu waliopeperusha bendera wakati ilitua.
Imechukua miaka minane kuunda ndege hiyo iliyo na uzito wa tani 53.3.

Tayari kuna kandarasi 17 za kujengwa ndege hiyo kutoka ndani ya China.
Sera ya China ya kusini mwa bahari mwa China inapingwa vikali na nchi kadhaa majirani.

0 comments: