Kura hiyo itaashiria mabadiliko ya kwanza ya uongozi nchini humo tangu mwaka 1944.
Baada ya wiki saba za uchelewesho kutokana na malalamiko ya kisheria yaliyofikishwa mahakamani na chama tawala cha Boakai cha Unity dhidi ya tume ya uchaguzi nchini humo, vituo vya kupigia kura vinatarajiwa kufunguliwa kuanzia saa mbili asubuhi saa za Liberia na kufungwa majira ya saa 12 jioni kwa ajili ya wapigakura milioni 2.1 waliandikishwa kupiga kura
Chama cha Weah cha Muungano kwa ajili ya mabadiliko ya kidemokrasi, Coalition for Democratic Change (CDC) kimewataka wapiga kura kutokunywa pombe kupita kiasi katika sikukuu ya Krismasi na kuamka mapema siku ya tarehe 26 kupiga kura zao katika kile mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ya taifa NEC, Francis Korkoya alichosema kuwa ni "kujitolea mhanga kwa ajili ya demokrasia yetu na nchi yetu."
Watachagua mrithi wa rais Ellen Johnson Sirleaf, anayetarajiwa kuondoka madarakani mwezi Januari baada ya miaka 12 akiwa katika uongozi wa juu wa taifa hilo la Afrika Magharibi, linaloibuka kutoka katika mavumbi ya vita vya wenyewe kwa wenyewe,(1989-2003) na pia kushughulikia hatua za kupambana na mzozo wa ugonjwa wa Ebola (2014-16).
DW SWAHILI.
0 comments: