Tuesday 26 December 2017

Hofu ya Urusi kukata nyaya za mawasiliano ya mtandao chini ya bahari


fisa wa cheo cha juu wa jeshi nchini Uingereza ameonya kuwa Urusi inaweza kusababisha madhara makubwa zaidi kwa uchumi ikiwa italenga nyaya za mawasiliano ya mitandao zinazopitia chini ya bahari.

Sir Stuart Peach, mkuu wa majeshi, alisema kuwa nyanya hizo zinaweza kukatwa au kuharibiwa.
Madai hayo yanazua maswali kadhaa:

    Hiki ni kitu Urusi inaweza kukifabnya?
    Ni kitu gani kitatokea ikiwa itafanya hivyo au ikiwa mtu mwingine atafanya hivyo?

Nyaya hizo ni za kufanyia nini?

Zinatumiwa katika mawasiliano ya mitandao kati ya ya nchi tofauti na mabara.

Nyaya zote hizo 428 zinachukua umbali wa kilomita milioni 1.1 na kuzunguka dunia nzima.

Kiwango kikubwa cha data husambazwa kote duniani nchini ya bahari kwa nyaya na zingine hjuwa nyembamba kama karatasi.
wa bahati mbaya, huku teknoljia yao ikiwa inategemewa sana, nyaya hizo zinaweza kuharibiwa. Nyaya hizo hufunikwa na plastiki, lakini nyingi bado zina upana wa sentimita tatu.

Majanga ya asili yanaweza kuziharibu na au hata meli ikitia nanga. Hicho ndicho kilitokea katika bandari ya Alexandria nchini Misri na kusababisha kukatwa mawasiliano kati ya Ulaya, Afrika na Asia.
Ni kwa nini wakuu ya jeshi wana hofu?

Mwandishi wa masuala ya ulinzi wa BBC Jonathan Beale anasema kuwa hofu ya Urusi kuweza kukata au kuharibu nyaya za chini ya bahari inazidi kuongezeka.

Nyambizi za Urusi zinazidi kuonekana sana bahari ya North Atlantic, hasa eneo lililo kati ya Grenland, Iceland na Uingereza.

Marshal Peach anasema kuwa Uingereza na washirika wake wa Nato wanakosa nyambizi, meli na ndege za kufanyia ujasusi.
i kitu gani kitatokea ikiwa nyaya hizo zitakatwa?

Keir Giles ambaye ni mtaalamu wa masuala ya vita vya mawasiliano vya Urusi, anasema kuwa hilo halina uwezekano wa kutokea kwa sababu linaweza pia kuiathiri Urusi, lakini ni kitu ambacho pia Urusi inaweza kukifanya.

Na ikiwa itatokea kutakuwa na madhara makubwa.

Anasema kuwa watu hata hawatakuwa na uwezi wa kuingia kwneye mtandao wa Facebook.

"Biashara ya kimataifa na malipo ya mashirika ya fedha hufanywa kupitia nyaya za chini ya bahari. Madhara ya uchumi yatakuwa ni makubwa."

Anaamini Urusi inataka kufahamu na kuacha kutegea sana mitandao na kubuni njia zake mbadala na kutaka kufahami pia kuhusu ni kipi kitatokea ikiwa mawasiliano ya mitandao yatavunjika.

0 comments: