Saturday, 3 February 2018

Uchimbaji mafuta ya Petroli mkoani Morogoro kuanza Septemba 2018
Serikali imesema mradi wa uchimbaji mafuta katika Kisima kilichoanishwa kuchimbwa kwenye eneo la kijiji cha Ipera Asilia, kwenye hifadhi tengefu ya bonde la Kilombero, mkoani Morogoro, unatarajiwa kuanza rasmi mwezi Septemba, 2018 ambapo kisima hicho kinakadiriwa kuwa na mafuta kuanzia lita milioni 180 hadi 200.

Akizungumza jana Februari 2, 2018 katika kipindi cha maswali na majibu kwenye kikao cha nne cha mkutano wa 10 wa Bunge mjini Dodoma, Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amesema kinachosubiriwa ni kibali kutoka Baraza la Mazingira nchini (NEMC) na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), ili uchimbaji huo uanze rasmi.

“Mkataba ulishasainiwa tangu mwaka 2012 kilihobaki ni utekelezaji wa uchimbaji na ugunduzi wa mafuta, mafuta yanayotarajiwa kuchimbwa kwenye eneo hilo yanafikia milionii 180 hadi 200, mtaji ni mkubwa na utakua na manufaa kwa wananchi wako na nchi kwa ujumla,” alisema na kuongeza.

“Kinachosubiriwa ni kibali cha mazingira kutoka NEMC na mamlaka ya TAWA, mwezi Julai mwaka huu tumehakikishiwa mkataba utapatikana na Septemba uchimbaji utaanza rasmi.”

Serikali kupitia shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) liliingia mkataba wa utafiti na uchimbaji wa gesi na uvunaji mafuta na Kampuni ya Mafuta na gesi ya Swala (Swala Oil), ambapo katika utekelezaji wa mkataba huo iligundulika kuwepo kwa wingi mafuta ya petrol na gesi katika vijiji vya Mtimbira.
TRA yazifungia hoteli tatu Mtwara kwa Kushindwa Kulipa Kodi
Mamlaka ya Mapato  TRA  imezifungia hotel tatu mkoani humo pamoja na kituo cha kuuza mafuta kwa kushindwa kulipa kodi .

Hotel zilizofungiwa ni Naf Beach, Naf blue, BNN pamoja na kituo cha Mnarani Petrol Station ambao kwa pamoja wanadaiwa zaidi ya Sh1bilioni ambazo ni malimbikizo ya madeni ya nyuma kwa kipindi cha miaka mitatu.

Ofisa mwandamizi wa huduma na elimu kwa mlipa kodi mkoa wa Mtwara,  Flavian Byabato amesema zoezi hilo ni endelevu kwa mkoa mzima.

“Ni madeni ambayo yametokana na ukaguzi kwa kipindi cha miaka mitatu nyuma, kikubwa walipe kodi..tunafungia kwa mambo mbalimbali kama malimbikizo ya madeni ya muda mrefu, matumizi sahihi ya mashine za EFD katika kutoa na kudai risiti sahihi inayoakisi gharama halisi ya malipo na kutii sheria  za kodi kama kutunza kumbukumbu,” amesema Byabato

Byabato amesema endapo wadaiwa watashindwa kulipa madeni yao watachukua hatua nyigine kama kukamata mali au kuwapeleka mahakamani kama hawatajitokeza kuomba na kuahidi ni lini watalipa madeni kwani hakuna aliyejitokeza kufanya hivyo.

Aidha amesema pia yapo maduka madogo ambayo yamefungiwa na kwa sasa wako wilayani Masasi wanaendelea na ukaguzi.

Friday, 2 February 2018

Serikali yabanwa madudu mkataba wa Mlimani City
Bunge limeitaka serikali kuhakikisha Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) anafanya ukaguzi wa kiuchunguzi na kiufanisi katika mikataba yote inayohusu mradi wa Mlimani City na kuwasilisha ripoti bungeni, baada ya kubaini dosari kubwa kwenye uendeshaji wa mradi huo.

Agizo hilo limetolewa ikiwa ni wiki mbili baada ya chombo hicho cha kutunga sheria kuukagua mradi huo jijini Dar es Salaam.

Katika ukaguzi wake, Bunge liligundua mbia wa mradi huo unaokihusisha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) amewekeza mtaji wa Dola za Kimarekani 75 (Sh. 150,000) kutoka mfukoni kwake.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Naghenjwa Kaboyoka, ndiye alitoa agizo kwa CAG kukagua mradi huo alipowasilisha bungeni mjini hapa jana taarifa ya shughuli za kamati yake kwa mwaka 2017.

Alisema upungufu uliobainika katika mradi huo unainyima serikali mapato stahiki na hivyo kuwa eneo mojawapo lenye matumizi mabaya ya fedha za umma.

Kaboyoka alisema kamati yake imebaini dosari kutokana na mradi wa ujenzi wa Mlimani City ulioanza Oktoba mosi, 2004 ukitakiwa kukamilika Septemba mosi, 2006 kwa makubaliano ya mkodishwaji na mkodishaji, kwa maana ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Kampuni ya Mlimani Holding Limited (MHL), kutokamilika mpaka sasa.

Alisema uchambuzi wa kamati yake katika ripoti ya CAG pamoja na mahojiano na uongozi wa UDSM, umebaini dosari kubwa katika usimamizi na uendeshaji wa mradi huo, hali ambayo inaipa serikali hasara.

Alizitaja dosari hizo kuwa ni pamoja na Dola 75 ambazo zilionyeshwa kama mtaji wa MHL ambao ni kinyume cha Sheria ya Uwekezaji ya Mwaka 1977 inayoelekeza kwamba, ili kibali cha uwekezaji kitolewe lazima mwekezaji awe na mtaji wa kutosha.

Mbunge huyo wa Same Mashariki (Chadema) alisema kamati yake pia imebaini Turnstar Holding Limited ni miongoni mwa wanahisa wa MHL na anamiliki hisa moja na kwamba kampuni hiyo imetoa mikopo kwa MHL jumla ya Dola za Marekani 49,027,840.

"Kamati ilipata mashaka kuhusu nia hiyo ya mbia huyu kwa kuwa MHL ana hisa 900 ambazo hazijauzwa na hivyo angenunua badala ya kukopesha. Kamati inaona mbia huyu ana lengo lake la kujinufaisha zaidi kwa kutoa mikopo kwa vile riba anayolipwa inatolewa kwenye mapato ghafi kabla ya kugawana faida," alisema.

Kaboyoka pia alibainisha kuwa kwa miaka 13 tangu mkataba huo uingiwe, mradi wa ujenzi wa hoteli ya nyota tatu yenye vyumba 100 bado haujaanza, kinyume cha makubaliano, hivyo kuongeza gharama za kumalizika kwa mradi. Pia mradi wa utengenezaji wa bustani ya wanyama na mimea (Botanical Garden) uliopaswa kwenda sawia na hoteli hiyo haujatekelezwa.

Aliongeza kuwa kumekuwapo ukiukwaji wa malipo ya pango la ardhi ya chuo ambapo vifungu cha 1.1(j) na 10.1 vya mkataba vinaeleza kuwa UDSM itapata asilimia 10 ya pango la mapato ghafi, lakini MHL imekuwa ikifanya malipo ya pango kwa chuo baada ya kutoa gharama za uendeshaji, hivyo kuikosesha serikali mapato stahiki kinyume cha mkataba.

Pia alisema wamebaini kukiukwa kwa kifungu cha 12.2(l) cha hati ya makubaliano ya mpangaji kinachomtaka MHL kutopangisha mtu yeyote ambaye hajathibitishwa na mpangishaji (UDSM).

Alisema ukaguzi wao umethibitisha kuwa MHL amekuwa akipangisha wapangaji wengine bila kupata kibali cha chuo hivyo kusababisha chuo kukosa taarifa sahihi za mapato ya kodi kutoka kwa wapangaji wake.

Kaboyoka alisema kamati hairidhishwi na mazungumzo yanayoendelea kati ya UDSM na MHL kwa kuwa mwekezaji huyo amekuwa akiyakataa mapendekezo yote yenye maslahi kwa pande zote mbili badala yake amekuwa akishikilia mapendekezo yenye maslahi kwake tu.

"Wakati huo MHL ameongeza eneo la maduka na maegesho ya magari ambayo hayakuwamo katika mkataba.

Kama hiyo haitoshi, mwekezaji ameshindwa kuanza utekelezaji wa ujenzi wa hoteli na Botanical Garden ambavyo vipo kwa mujibu wa mkataba," Kaboyoka alisema.

Kigogo wa PAC huyo alisema mapitio ya mkataba yamebainisha kuwa hauelezi hali ya ugawanaji mali pindi mkataba utakapomalizika (miaka 50 au 85) kwa kuwa hakuna makubaliano rasmi yanayoeleza mgawanyo wa mali na miundombinu itakayokuwapo pindi mkataba utakapoisha.

Alibainisha kuwa athari ya jambo hilo ni kuwa kuna uwezekano mkubwa kutokea mvutano wa kisheria pindi mkataba huo utakapofika ukomo.

Kaboyoka alisema dosari nyingine ni kuhusu ushiriki wa serikali kupitia Kituo cha Uwekezaji (TIC) ambapo kituo hicho na MHL wamekuwa wakibadilisha muda wa utekelezaji wa mradi mara kwa mara kwa kumwongeza mwekezaji muda wa kukamilisha mradi bila kukihusisha chuo.

"Kwa mfano, mkataba wa kwanza ulisainiwa Februari 27, 2006 na kumwongeza mwekezaji kipindi cha utekelezaji wa mradi hadi Oktoba 30, 2009. Mkataba wa pili ulisainiwa Julai 13, 2007 kwa kuongeza muda wa utekelezaji hadi Novemba 30, 2013 na mkataba wa tatu ulisainiwa Desemba 10, 2014 ambao uliongeza muda wa utekelezaji wa mradi huo hadi Desemba 31, 2019," alisema.

Kaboyoka pia alisema mkataba unaonyesha kuwa zilitakiwa kujengwa nyumba 50 za kuishi (house estate/villas) lakini kamati yake ilipotembelea mradi huo zilizonekana nyumba 45 na nyumba moja yenye vyumba viwili vilivyotenganishwa na milango miwili.

Kutokana na dosari hizo, Kaboyoka alisema mradi wa Mlimani City unapaswa uangaliwe kwa kina kuanzia mkataba wa kwanza hadi hapo ulipofika sasa.

Tuesday, 9 January 2018

Hii ndio benki mpya iliyopewa leseni ya biashara na Benki Kuu ya Tanzania
Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imetoa taarifa kwa kwa umma kuwa, imetoa leseni ya biashara kwa benki mpya yenye jina, Guaranty Trust Bank (Tanzania) Limited.

Leseni hiyo inatoa kibali kwa taasisi hiyo kutoa huduma za kibenki nchini Tanzania kama benki ya kibishara na imetolewa kuanzia Januari 5, 2018.

Makao Makuu ya Benki hiyo yanapatikana Kitalu namba 4, Regent Estate, Barabara ya Bagamoyo, jijini Dar es Salaam.

Hatua hiyo ya Benki Kuu imekuja siku chache tangu ilipozifutia leseni za biashara, benki 5 ambazo ni Covenant Bank, Efatha Bank, Njombe Community Bank, Kagera Farmers’ Cooperative Bank, na Meru Community Bank.

Benki Kuu ilizifungia benki hizo kutokana na kushuka kwa mtaji.

Thursday, 4 January 2018

Urafiki watangaza kiama kwa wapangaji wake
Uongozi wa Kiwanda  cha Urafiki  umetangaza kiama kwa wapangaji wake ukiwataka kulipa kodi la sivyo wataondolewa pasipo huruma wala kuangalia hadhi ya mtu.

Akizungumza na Mwananchi leo Januari 4, 2018, naibu meneja mkuu wa kiwanda hicho, Shadrack Nkelebe amesema notisi ya siku 30 waliyotoa kwa wapangaji hao katika nyumba zilizopo Urafiki Kota, Ubungo imekwisha.

Desemba 21 mwaka jana uongozi wa kiwanda hicho ulitangaza kiama kwa wapangaji zaidi ya 160 ukiwataka kulipa kodi la sivyo watawaondoa.

Miongoni mwa walioponea chupuchupu kuondolewa katika nyumba hizo ni meya wa zamani wa Halmashauri ya Kinondoni, Salum Londa aliyelipa Sh18milioni huku mchezaji wa zamani wa Yanga, Zamoyoni Mogella aliyekuwa akidaiwa Sh5milioni, ikielezwa ataondolewa wakati wowote.

“Wiki ijayo tutaanza kuwatoa wapangaji wetu ambao wamekuwa sugu kulipa madeni ya kodi, tumefanya ubinadamu, tumewaita viongozi wa serikali za mitaa ili shughuli ya kuwatoa ikianza wasishangae,” amesema Nkelebe,

“Wapo ambao wameanza kuja kulipa na wapo ambao wameanza kukimbia, hao tutawatafuta, hatutakubali kodi yetu waondoke nayo. Wale  ambao mpaka sasa hawajalipa, tunawashauri tu walipe wasije kupata adha ya kutolewa kwa vitu vyao nje.”

Operesheni ya kuwaondoa inafanywa na Kampuni ua Udalali ya Yono ambayo mwezi uliopita uliwaondoa wapangaji wa nyumba hizo wenye ofisi kwa kuchukua vifaa ili kufidia madeni yao, huku  baadhi Nkelebe akisema wamekwisha kuanza kulipa.

“Wapo ambao tayari wamelipa na kuchukua vitu vyao lakini wapo ambao hawajafanya hivyo. Tunataka fedha hizo ili ziweze kuingizwa katika shughuli zetu kama za kununua pamba,  kulipa wafanyakazi, ukarabati wa majengo na mashine,” amesema Nkelebe.
Breaking News: BOT yazifutia leseni Benki Tano
Benki Kuu ya Tanzania(BoT) imezifutia  leseni ya kufanya biashara benki tano na kuziweka chini ya ufilisi.

Taarifa iliyotolewa leo Alhamisi na BoT imezitaja benki hizo kuwa ni Covenant Bank For Women (Tanzania) Limited, Efatha Bank Limited, Njombe Community Bank Limited, Kagera Farmers' Cooperative Bank Limited, na

Meru Community Bank Limited.

BoT imeeleza kuwa imefanya hivyo kwa mamlaka iliyopewa chini ya kifungu cha 56(1)(g), 56(2) (a), (b) na (d), 58(2)(i), 11(3)(c) na (j), 61(1) na 41(a) cha Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006, Benki Kuu ya Tanzania imeamua kuzifunga; kusitisha shughuli zake zote za kibenki; kufuta leseni zake za biashara ya kibenki; na kuziweka chini ya ufilisi.

“Kwa mamlaka iliyopewa chini ya kifungu Na. 41(a) cha Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006; Benki Kuu ya Tanzania imeiteua Bodi ya Bima ya Amana (The DEPOSIT INSURANCE BOARD) kuwa mfiiisi kuanzia tarehe 04 Januari 2018,” imeeleza taarifa hiyo.”

“Uamuzi huu umechukuliwa baada ya Benki Kuu ya Tanzania kujiridhisha kuwa benki hizi zina upungufu mkubwa wa mtaji kinyume na matakwa ya Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006 na kanuni zake. Upungufu huo wa mtaji unahatarisha usalama wa sekta ya fedha na kwamba kuendelea kutoa huduma za kibenki kwa benki hizo kunahatarisha usalama wa amana za wateja wake.”

Taarifa hiyo imeeleza kuwa BoT inapenda kuuhakikishia umma kuwa itaendelea kulinda maslahi ya wenye amana katika mabenki kwa lengo la kuleta uhimilivu katika sekta ya fedha.

Wednesday, 3 January 2018

Bei Mpya Elekezi za Mafuta ya Petroli kutoka EWURA
January 3, 2017 Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) imetoa bei mpya elekezi za Mafuta ya Petrol, Diesel pamoja na mafuta ya Taa kwa Mwaka. Bei hizi zitaanza kutumika kuanzia January 3.

  
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Godwin Samwel, bei zitakazoanza kutumika leo Petroli imezidi kupanda bei kwa shilingi 8/lita, kupanda huku kumetokana na mabadiliko ya bei katika soko la Dunia.
 
Pamoja na kutaja bei kikomo za bidhaa mbalimbali za mafuta nchi nzima, EWURA wametaja mambo muhimu ya kuzingatia   kama ifuatavyo.
  • Bei za jumla na rejareja kwa mafuta ya aina zote yaliyoingizwa nchini kupitia bandari ya Dar es Salaam, yaani Petroli, Dizeli na Mafuta ya Taa zimeongezeka ikilinganishwa na toleo lililopita la tarehe 6 Disemba 2017. Kwa mwezi Januari 2018, bei za rejareja za Petroli, Dizeli na Mafuta ya Taa zimeongezeka kwa Shilingi 8/lita (sawa na asilimia 0.35), Shilingi 34/lita (sawa na asilimia 1.71) na Shilingi 89/lita (sawa na asilimia 4.57) sawia. Vilevile, kwa kulinganisha na toleo la mwezi uliopita, bei za jumla za Petroli, Dizeli na Mafuta ya Taa zimeongezeka kwa Shilingi 7.56/lita (sawa na asilimia 0.37), Shilingi 33.97/lita (sawa na asilimia 1.81) na Shilingi 88.73/lita (sawa na asilimia 4.85) sawia. Ongezeko la bei za mafuta ya Petroli, Dizeli na Mafuta ya Taa limetokana na ongezeko la bei za mafuta hayo katika soko la dunia na ongezeko la gharama za usafirishaji (BPS Premiums).
  • Bei za jumla na rejareja kwa mafuta ya Petroli na Dizeli yaliyoingizwa nchini kupitia bandari ya Tanga nazo zimeongezeka ikilinganishwa na toleo lililopita la tarehe 6 Disemba 2017. Bei za Mafuta ya Taa hazijabadilika kwa sababu hakuna Mafuta ya Taa yaliyoingizwa nchini kupitia bandari ya Tanga katika mwezi wa Disemba 2017. Katika toleo hili, bei za rejareja za Petroli na Dizeli kwa Mikoa ya Kaskazini zimeongezeka kwa Shilingi 60/lita (sawa na asilimia 2.78) na Shilingi 69/lita (sawa na asilimia 3.47), sawia. Aidha, kwa kulinganisha na toleo la mwezi uliopita, bei za jumla za Petroli na Dizeli zimeongezeka kwa Shilingi 59.68/lita (sawa na asilimia 2.93) na Shilingi 69.02/lita (sawa na asilimia 3.67). Ongezeko la bei za mafuta ya Petroli na Dizeli katika mkoa wa Tanga linatokana na kuongezeka kwa bei za mafuta hayo katika soko la dunia na kuongezeka kwa gharama za usafirishaji (BPS premiums).
  • Ifahamike kwamba, sehemu kubwa ya shehena za mafuta yaliyopokelewa katika bandari ya Dar es Salaam ni zile zenye bei za soko la dunia za mwezi Oktoba 2017 wakati shehena iliyopokelewa katika bandari ya Tanga ni ya bei za soko la dunia za mwezi Novemba 2017. Bei za mafuta katika soko la dunia kwa mwezi Novemba 2017 ziko juu kwa zaidi ya asilimia 6 ikilinganishwa na bei za mwezi Oktoba 2017.
  • Mamlaka inapenda kuukumbusha umma kwamba bei kikomo za mafuta kwa eneo husika, zinapatikana pia kupitia simu za mkononi kwa kupiga namba *152*00# na kisha kufuata maelekezo. Huduma hii ni bure na inapatikana kupitia mitandao yote ya simu za mkononi hapa nchini.
  • Kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta ya mwaka 2015, bei za bidhaa za mafuta ya petroli zitaendelea kupangwa na soko. EWURA itaendelea kuhamasisha ushindani kwa kutoa taarifa za bei kikomo za bidhaa za mafuta. Taarifa hizi zina lengo la kuwasaidia wadau kufanya maamuzi stahiki kuhusu manunuzi ya bidhaa za mafuta.
  • Kampuni za mafuta ziko huru kuuza bidhaa za mafuta ya petroli kwa bei ya ushindani mradi tu bei hizo zisivuke bei kikomo (price cap) kama ilivyokokotolewa na kanuni (formula) iliyopitishwa na EWURA na ambayo ilichapishwa katika Gazeti la Serikali Na. 216/2017 la mwezi Mei 2017.
  • Vituo vyote vya mafuta vinatakiwa kuchapisha bei za bidhaa za mafuta katika mabango yanayoonekana bayana na yakionesha bei ya mafuta, punguzo, vivutio vya biashara au promosheni zinazotolewa na kituo husika. Pale ambapo inawezekana kuchagua, wateja wanashauriwa kununua bidhaa za mafuta katika vituo vinavyouza mafuta kwa bei nafuu zaidi ili kushamirisha ushindani. Ni kosa kuuza mafuta bila kuweka mabango ya bei inayoonekana vizuri kwa wateja. Adhabu kali itatolewa kwa kituo husika kwa kutotekeleza matakwa ya kisheria kwa mujibu wa kanuni husika.
  • Wauzaji wa mafuta ya petroli wanatakiwa kutoa risiti za mauzo kutoka kwenye mashine za EFPP (Electronic Fiscal Pump Printers) na Wanunuzi wahakikishe wanapata stakabadhi hizo za malipo zinazoonyesha jina la kituo, tarehe, aina ya mafuta yaliyonunuliwa na bei kwa lita. Stakabadhi hizo za malipo zitatumika kama kidhibiti kwa wanunuzi wa mafuta endapo kutajitokeza malalamiko ya aidha kuuziwa mafuta kwa bei ya juu kuliko bei kikomo au kuuziwa mafuta  yasiyo na kiwango cha ubora kinachofaa, na pia, risiti hizo zitasaidia kurahishisha ukusanyaji wa kodi za Serikali zitokanazo na mafuta ya petroli.
A: BEI ZA REJAREJA
Mji
Bei Kikomo
Petroli (Shs/Lita) Dizeli (Shs/Lita) Mafuta Ya Taa (Shs/Lita)
Dar es Salaam                2,167               2,018                    2,031 
Arusha                2,263               2,115                    1,995 
Arumeru (Usa West)                 2,263                2,115                     1,995 
Karatu                 2,281                2,134                     2,013 
Monduli                 2,268                2,121                     2,000 
Monduli-Makuyuni                 2,273                2,125                     2,005 
Ngorongoro (Loliondo)                 2,347                2,200                     2,079 
Kibaha                2,172               2,023                    2,036 
Bagamoyo                 2,178                2,029                     2,042 
Kisarawe                 2,175                2,025                     2,038 
Mkuranga                 2,177                2,028                     2,041 
Rufiji                 2,195                2,046                     2,059 
Dodoma                2,226               2,077                    2,090 
Bahi                 2,233                2,084                     2,097 
Chemba                 2,252                2,103                     2,116 
Kondoa                 2,259                2,109                     2,122 
Kongwa                 2,223                2,074                     2,087 
Mpwapwa                 2,227                2,078                     2,091 
Iringa                2,231               2,082                    2,095 
Kilolo                 2,236                2,087                     2,099 
Mufindi (Mafinga)                 2,241                2,092                     2,105 
Njombe                2,259               2,110                    2,123 
Njombe (Kidegembye)                 2,280                2,131                     2,144 
Ludewa                 2,297                2,148                     2,161 
Makete                 2,290                2,141                     2,154 
Wanging’ombe (Igwachanya)                 2,257                2,108                     2,121 
Bukoba                2,382               2,233                    2,246 
Biharamulo                 2,357                2,207                     2,220 
Karagwe (Kayanga)                 2,399                2,249                     2,262 
Kyerwa (Ruberwa)                 2,404                2,255                     2,268 
Muleba                 2,382                2,233                     2,246 
Ngara                 2,348                2,199                     2,211 
Misenyi                 2,391                2,241                     2,254 
Geita                2,332               2,183                    2,196 
Bukombe                 2,321                2,172                     2,185 
Chato                 2,353                2,204                     2,217 
Mbogwe                 2,370                2,221                     2,234 
Nyang’hwale                 2,347                2,198                     2,211 
Kigoma                2,398               2,249                    2,262 
Uvinza (Lugufu)                 2,410                2,261                     2,274 
Buhigwe                 2,387                2,238                     2,251 
Kakonko                 2,355                2,206                     2,219 
Kasulu                 2,384                2,235                     2,248 
Kibondo                 2,363                2,213                     2,226 
Moshi                2,253               2,105                    1,984 
Hai (Bomang’ombe)                 2,256                2,108                     1,988 
Mwanga                 2,246                2,098                     1,977 
Rombo (Mkuu)                 2,269                2,122                     2,001 
Same                 2,239                2,091                     1,971 
Siha (Sanya Juu)                 2,259                2,112                     1,991 
Lindi                2,226               2,077                    2,090 
Lindi-Mtama                 2,244                2,095                     2,108 
Kilwa Masoko                 2,201                2,052                     2,065 
Liwale                 2,247                2,098                     2,111 
Nachingwea                 2,255                2,106                     2,119 
Ruangwa                 2,257                2,108                     2,121 
Babati                2,297               2,149                    2,029 
Hanang (Katesh)                 2,307                2,160                     2,039 
Kiteto (Kibaya)                 2,312                2,165                     2,044 
Mbulu                 2,310                2,162                     2,041 
Simanjiro (Orkasumet)                 2,329                2,181                     2,061 
Musoma                2,346               2,196                    2,209 
Musoma Vijijini (Busekela)                  2,386                2,237                     2,250 
Rorya (Ingirijuu)                 2,354                2,205                     2,218 
Rorya (Shirati)                 2,389                2,240                     2,253 
Bunda                 2,337                2,187                     2,200 
Butiama                 2,342                2,193                     2,206 
Serengeti (Mugumu)                 2,391                2,242                     2,255 
Tarime                 2,357                2,207                     2,220 
Tarime (Kewanja/Nyamongo)                 2,361                2,212                     2,225 
Mbeya                2,274               2,125                    2,138 
Chunya                 2,284                2,134                     2,147 
Chunya (Makongolosi)                 2,298                2,149                     2,162 
Ileje                 2,287                2,138                     2,151 
Kyela                 2,290                2,141                     2,154 
Mbarali (Rujewa)                 2,258                2,109                     2,122 
Mbozi (Vwawa)                 2,284                2,134                     2,147 
Momba (Chitete)                 2,292                2,143                     2,156 
Rungwe (Tukuyu)                 2,283                2,134                     2,147 
Morogoro                2,192               2,043                    2,056 
Mikumi                 2,208                2,059                     2,072 
Kilombero (Ifakara)                 2,230                2,081                     2,094 
Kilombero (Mlimba)                 2,252                2,103                     2,116 
Kilombero (Mngeta)                 2,242                2,092                     2,105 
Ulanga (Mahenge)                 2,241                2,091                     2,104 
Malinyi                 2,251                2,102                     2,115 
Kilosa                 2,211                2,061                     2,074 
Gairo                 2,211                2,061                     2,074 
Mvomero (Wami Sokoine)                 2,203                2,054                     2,066 
Turiani                 2,217                2,068                     2,081 
Mtwara                2,240               2,090                    2,103 
Nanyumbu (Mangaka)                 2,288                2,139                     2,152 
Masasi                 2,265                2,116                     2,129 
Newala                 2,272                2,122                     2,135 
Tandahimba                 2,265                 2,115                     2,128 
Mwanza                2,317               2,168                    2,181 
Kwimba                 2,353                2,204                     2,217 
Magu                 2,325                2,176                     2,189 
Misungwi                 2,323                2,173                     2,186 
Sengerema                 2,350                2,200                     2,213 
Ukerewe                 2,377                2,227                     2,240 
Sumbawanga                2,340               2,191                    2,203 
Kalambo (Matai)                 2,347                2,198                     2,211 
Nkasi (Namanyele)                 2,353                2,204                     2,217 
Katavi (Mpanda)                 2,375                2,226                     2,238 
Mlele (Inyonga)                 2,353                2,204                     2,217 
Songea                2,291               2,141                    2,154 
Mbinga                 2,324                2,175                     2,188 
Namtumbo                 2,320                2,171                     2,183 
Nyasa (Mbamba Bay)                 2,326                2,177                     2,190 
Tunduru                 2,349                2,200                     2,213 
Shinyanga                2,296               2,147                    2,160  
Kahama                 2,310                2,160                     2,173 
Kishapu                 2,324                2,175                     2,188 
Simiyu (Bariadi)                 2,337                2,188                     2,201 
Busega (Nyashimo)                 2,330                2,181                     2,194 
Itilima (Lagangabilili)                 2,340                2,191                     2,204 
Maswa                 2,329                2,180                     2,192 
Meatu (Mwanhuzi)                 2,336                2,187                     2,199 
Singida                2,258               2,109                    2,121 
Iramba                 2,270                2,121                     2,134 
Manyoni                 2,242                2,093                     2,106 
Ikungi                 2,253                2,104                     2,117 
Mkalama (Nduguti)                 2,282                2,133                      2,146 
Tabora                2,321               2,172                    2,185 
Igunga                 2,275                2,126                     2,139 
Kaliua                 2,339                2,190                     2,203 
Ulyankulu                 2,333                2,184                     2,197 
Nzega                 2,286                2,137                     2,149 
Sikonge                 2,333                2,184                     2,197 
Urambo                 2,334                2,185                     2,198 
Tanga                2,206               2,059                    1,938 
Handeni                 2,227                2,079                     1,959 
Kilindi                 2,242                2,094                     1,974 
Korogwe                 2,219                2,071                     1,950 
Lushoto                 2,228                2,080                     1,960 
Mkinga (Maramba)                 2,213                2,066                     1,945 
Muheza                 2,211                2,064                     1,943 
Pangani                 2,213                2,066                     1,945 
B: BEI ZA JUMLA 
Bei za Jumla – DSM Petroli (Shs/Lita) Dizeli  (Shs/Lita) Mafuta ya Taa (Shs/Lita)
Bei Kikomo 2,056.41 1,907.12 1,920.00

 

Bei za Jumla – TANGA Petroli (Shs/Lita) Dizeli  (Shs/Lita) Mafuta ya Taa (Shs/Lita)
Bei Kikomo 2,095.46 1,947.93 1,827.17
   Mhandisi Godwin Samwel
KAIMU MKURUGENZI MKUU
  EWURA