Mamlaka ya Mapato TRA imezifungia hotel tatu mkoani humo pamoja na kituo cha kuuza mafuta kwa kushindwa kulipa kodi .
Hotel
zilizofungiwa ni Naf Beach, Naf blue, BNN pamoja na kituo cha Mnarani
Petrol Station ambao kwa pamoja wanadaiwa zaidi ya Sh1bilioni ambazo ni
malimbikizo ya madeni ya nyuma kwa kipindi cha miaka mitatu.
Ofisa
mwandamizi wa huduma na elimu kwa mlipa kodi mkoa wa Mtwara, Flavian
Byabato amesema zoezi hilo ni endelevu kwa mkoa mzima.
“Ni
madeni ambayo yametokana na ukaguzi kwa kipindi cha miaka mitatu nyuma,
kikubwa walipe kodi..tunafungia kwa mambo mbalimbali kama malimbikizo
ya madeni ya muda mrefu, matumizi sahihi ya mashine za EFD katika kutoa
na kudai risiti sahihi inayoakisi gharama halisi ya malipo na kutii
sheria za kodi kama kutunza kumbukumbu,” amesema Byabato
Byabato
amesema endapo wadaiwa watashindwa kulipa madeni yao watachukua hatua
nyigine kama kukamata mali au kuwapeleka mahakamani kama hawatajitokeza
kuomba na kuahidi ni lini watalipa madeni kwani hakuna aliyejitokeza
kufanya hivyo.
Aidha amesema pia yapo maduka madogo ambayo yamefungiwa na kwa sasa wako wilayani Masasi wanaendelea na ukaguzi.
0 comments: