Shirikisho
la Soka Tanzania (TFF) limeahidi kuendeleza viwanja tisa nchini
kufuatia kuongezeka kwa dau la pesa za Maendeleo na Kujiendesha
zinazotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani FIFA kuanzia mwaka
2019 .
Kauli
hiyo imetolewa jana jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari Utamaduni
Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe alipokuwa akizungumza na vyombo
vya habari kuhusu mambo mbalimbali serikali iliyojadili na Rais wa FIFA
Gianni Infantino alipokuwa nchini kwa mkutano wake hivi karibuni.
‘’Rais
wa FIFA alieleza kuongeza mara nne ya kiwango cha pesa za maendeleo na
kujiendesha walizokuwa wanatoa kwa mashirikisho kama TFF mpaka kufikia
Dola Milioni Moja na Laki Mbili na Nusu kwa mwaka na kusema pesa hizo
ndiyo zitumike kuendeleza viwanja vya michezo kwani uwepo wa viwanja
ndio unaosaidia kukuza vipaji vya soka,’’alisema Dkt.Mwakyembe.
Akiendelea
kuzungumza katika mkutano huo na waandishi wa habari Waziri Mwakyembe
alisisitiza kuwa Rais huyo wa FIFA ametoa msisitizo wa kutokuwa na
huruma kwa kiongozi yoyote wa shirikisho atakayekuwa na matumizi mabaya
ya pesa pamoja na kufanya udanganyifu kwani yeye yuko mstari wa mbele
kupinga ufisadi katika sekta ya maendeleo ya Soka duniani.
Pamoja
na hayo nae Rais wa TFF Bw. Wallace Karia alitoa ufafanuzi wa hali ya
kifedha kwa shirikisho na kueleza kufuatia kuwepo na matatizo katika
shirikisho hilo .FIFA ilikuwa imesitisha kuwapatia fedha hizo za
maendeleo za kujiendesha tangu mwaka 2015 lakini baada ya kuingia
uongozi mpya FIFA wameridhika nao na wameshaupa utaratibu wa kufuatilia
fedha hizo.
‘’Rais
wa FIFA alitueleza kuwa fedha hizo ziko salama nchini Zurich ni kwamba
tu hazikuwa zimeruhusiwa kuingia nchini na kwa sasa tumeshaanza mchakato
wa kufuatilia fedha hizo kwa kuzingatia maelekezo ya FIFA hivyo basi
tutakapo pata fedha hizo Shirikisho litaendeleza baadhi ya miradi
ambayo tumekwisha iandaa,’’alisema Bw. Karia.
Pamoja
na hayo rais huyo alitoa wito wa wakazi wa jiji la Tanga waliovamia
eneo linalotarajia kujengwa Technical Center ya mchezo wa soka
waondoke mara moja kabla hawajachukuliwa hatua.
0 comments: