Taarifa za kifo cha mwanafunzi Aquillina Akwilini aliyepigwa risasi
kifuani na Polisi na kupoteza maisha jana February 16, 2018 akiwa kwenye
daladala zinaendelea kuenea kwenye mitandao ya kijamii.
Inaelezwa kuwa tukio hilo lilitokea wakati Askari Polisi wakiwatawanya
wafuasi wa upinzani waliokuwa wakifanya maandamano katika eneo la
Mkwajuni jijini Dar es Salaam.
Watu maarufu mbalimbali wameandika kwenye mitandao yao ya kijamii na
kuonesha kuguswa na tukio hilo la kuuawa kwa Binti huyo, ikiwa ni pamoja
na Mwanamuziki Shilole, Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe na Mwandishi
wa Habari za Michezo Edo Kumwembe.
0 comments: