Sunday 25 February 2018

Mlinzi wa Simba aanza rasmi mazoezi

Mlinzi wa kati wa timu ya Simba Salim Mbonde amepona majeraha yake na ameanza rasmi mazoezi chini ya Kocha wa Viungo 'Fitness Coach' Mohammed Hbibi kwaajili ya kujiandaa kuanza kucheza.

Taarifa ya klabu hiyo leo imebainisha kuwa mlinzi huyo ataendelea na mazoezi hayo chini ya uangalizi wa daktari wa timu hiyo Yassin Gembe na anatarajiwa kuwa kamili kucheza hivi karibuni.

Salim Mbonde alisajiliwa na Simba kwenye dirisha kubwa la usajili msimu huu ambapo amekuwa akicheza kwa kupishana na walinzi wengine ndani ya timu hiyo wakiwemo Juuko Murshid, Mlipili na Nyoni.

Klabu ya SImba inaendelea na maandalizi ya mchezo wake wa raundi ya 19 ligi kuu soka Tanzania Bara dhidi ya Mbao FC. Mchezo huo utapigwa kesho kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.

Baada ya mchezo huo Simba itaendelea na maandalizi ya mchezo wake wa kimataifa kombe la shirikisho barani Afrika utakaopigwa Machi 6 mwaka huu dhidi ya Al Masry ya Misri.

0 comments: