Makamu wa Rais, Bi Samia Suluhu Hassan (katikati) akiwa na wasanii Nandy na Aslay.
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan jana jioni aliwakaribisha nyumbani kwake wasanii wa Bongo Fleva,
Aslay Isihaka ‘Dogo Aslay’ na Faustina Charles maarufu kama Nandy kwa
ajili ya mazungumzo mafupi na chakula cha jioni.
Katika mazungumzo yake na wasanii hao, Bi Samia alieleza kuvutiwa sana
na marudio ya kibao cha SUBALKHERI kilichorudiwa na wakali hao wa Bongo
Fleva hivi karibuni na kuwapa wosia wa kuendelea kufanya kazi nzuri
zaidi na kujiepusha na makundi mabaya.
0 comments: