Sunday, 25 February 2018

Mlanguzi wa mihadarati, Washington Prado Álava wa Ecuador, ahamishiwa Marekani

Mwanamume mmoja ambaye anatuhumiwa kuingiza hadi Marekani zaidi ya tani 250 ya dawa za kulevya aina ya cocaine katika kipindi cha muongo mmoja uliopita, amehamishiwa Marekani kutoka Colombia.
Waendesha mashtaka wanasema kuwa, Washington Prado Álava, raia wa Ecuador, alikuwa mlanguzi mkuu wa mihadarati kote Amerika.
Pia anasemekana kuamuru kuuwawa kwa majaji, waendesha mashtaka na maafisa wa polisi nchini Ecuador.

Bwana Prado Álava alifahamika nchini Colombia kama Pablo Escobar, wa Ecuador, jina la kinara mmoja sugu wa genge maarufu liitwalo Medellín, ambaye aliuwawa mwaka 1993.
Nchini Colombia, alijaribu sana kujiunga na kundi la mrengo wa kushoto la waasi la Farc, kabla kundi hilo kutia saini na mapatano na serikali ya nchi hiyo, ili kukomesha mapigano.
Waendesha mashtaka nchini Colombia, wanasema kwamba nia yake kuu ilikuwa kupata cheo cha juu ndani ya kundi hilo na kisha kuchukua udhibiti wa sheria ya taifa hilo.
Kundi hilo la Farc lilisababisha uhasama wa muda mrefu sana nchini Colombia kwa zaidi ya miongo mitano.
"Washington Prado Álava anadhaniwa kuwa kiongozi mkuu zaidi wa ulanguzi wa mihadarati katika miaka ya hivi karibuni, na amekuwa akilengwa na Marekani," waendesha mashtaka walisema hayo katika taarifa waliyoitoa.
Bwana Prado Álava, anasemekana kuendesha biashara hiyo yake haramu nchini Ecuador na kisiwani Colombia, pwani ya bahari ya Pacific.
inasdemekana kuwa maboti yake kadhaa inayoenda kwa kasi, yalitumika mara kwa mara kusafirisha Coccaine hadi katikati mwa Amerika na Mexico, na kutoka hapo, dawa hizo za kulevya ziliwasilisha hadi katika mpaka wa Marekani.
Bwana Prado Álava alikamatwa Aprili 2017alipokuwa akisafiri kutembelea familia yake katika mji wa Cali nchini Colombia.
Shirika la Marekani la kupambana na mihadarati USDEA, iliipa utawala wa Colombia na vidokezo muhimu vya ki- intelijensia, iliyosababisha kukamatwa kwake kwa pamoja na wanachama wengine watatu wa genge hilo.
Siku ya Jumamosi, aliondolewa ndani ya gereza alimokuwa amezuiliwa katika mji mkuu Bogotá, na akawekwa ndani ya ndege ili kukabiliwa na sheria nchini Marekani.
Askari 50 walihusika katika operesheni ya kumhamishia Marekani, Utawala nchini Colombia umesema.

0 comments: