Chama kinachotawala nchini China kimependekeza kuondoa sehemu katika
katiba ambayo inaweka muhula wa rais kuwa mihula miwili ya miaka mitano
kila muhula.
Hatua hiyo itaruhusu rais wa sasa Xi Jinping kubaki kiongozi baada ya
muhula wake kukamilika, Kumekuwa na uvumi kuwa Bw Xi ataongeza muhula
wake hadi kupita mwaka 2023.
Kamati kuu wa chama mwaka uliopita iliboresha nguvu za Xi na kumfanya
kuwa kiongozi mwenye nguvu zaidi tangu uongozi wa Rais Mao Zedong.
Fikra zake pia zilijumuishwa katika katiba ya chama, na kwenda kinyume na ratiba hakuna mrithi aliyetangazwa.
Kamati kuu ya chama cha kikomunisti ilipendekeza kuondoa sehemu
inayosema kuwa Rais na Makamu wa Rais wa China wanastahili kuhudumu
kipindi kisichozidi mihula miwili kulingana na katiba.
Kamati hiyo haikutoa taarifa za kina lakini taarifa kamili zinatarajiwa
kutolewa, Hatua hiyo inajiri wakati maafisa ya vyeo vya juu ambao wako
katika kamati kuu wanatarajiwa kukutana siku ya Jumatatu mjini Beijing.
Bw Xi amekuwa madarakani tangu mwaka 2013 na chini ya mfumo wa sasa alistahili kuondoka madarakani mwaka 2023.
0 comments: