Ujumbe wa Korea Kaskazini unaoongozwa na jenerali wa jeshi mwenye utata
umevuka na kuingia Korea Kusini kwa sherehe za kufungwa mashindano ya
olimpiki ya msimu wa baridi huko Pyeongchang.
Jenerali Kim Yong-chol analaumiwa kwa kuzamisha meli ya vita ya Korea
Kusini mwaka 2010 ambapo wanajeshi 46 waliuawa. Korea Kaskazini inakana
kuhusika.
Familia za waathiriwa na wabunge kadhaa wa Korea Kusini walifanya maandamano wakijaribu kuzuia ziara hiyo kwenye mpaka.
Ziara hiyo inafanyika wakati kuna kuboreka kwa uhusiano kati ya Korea
hizo mbili, Wakati wa mashindano ya olimpiki Korea Kaskazini na Kusini
walitembea pamoja chini ya bendera moja wakati wa sherehe za ufunguzi na
baadaye wakawa na kikosi cha pamoja na wanawake wa timu ya magongo.
Hata hivyo wataalamu wanaonya kuwa yanayofanaika sasa hayamalizi kikomo
misukosuko ya kieneo hasa kufuatia majaribio ya nyuklia na ya makombora
yanayofanywa na Korea Kaskazini.
Ujumbe wa Marekani kwenye mashindano hayo unaojumuisha binti wa rais
Donald Trump Ivanka, umekana kukutana na maafisa wa Korea Kaskazini.
Siku ya Ijumaa Marekani ilitangaza awamu mpya ya vikwazo dhidi ya korea
Kaskazini, Rasi ya Korea imegawanyika tangu vita vya miaka 1950 na pande
zote mbili hazijawai kuwa na makubaliano ya mkataba wowote.
0 comments: