Rais wa Tanzania John Magufuli ameviagiza vyombo vya dola kuchunguza na
kuwachukulia hatua waliosababisha kifo cha mwanafunzi wa chuo cha
usafirishaji Tanzania, NIT, Akwilina Akwiline.
"Nimesikitishwa sana na kifo cha mwanafunzi Akwilina Akwilini wa Chuo
cha Usafirishaji (NIT). Natoa pole kwa familia,ndugu,wanafunzi wa NIT
na wote walioguswa na msiba huu. Nimeviagiza vyombo vya dola kufanya
uchunguzi na kuwachukulia hatua za kisheria waliosababisha tukio hili,"
Rais Magufuli aliandika kwenye mtandao wa Twitter.
Mwanafunzi huyo
ambaye jina lake na picha vilisambazwa katika mitando ya kijamii
alipigwa risasi akiwa ndani ya basi dogo maarufu kama daladala jijini
Dar es salaam, siku ya Ijumaa majira ya jioni, ikiwa siku moja kabla ya
uchaguzi mdogo wa eneo bunge la kinondoni kufanyika.
Walioshuhudia wanasema kuwa maafisa wa polisi walitumia vitoa machozi
na risasi katika harakati za kuwatawanya mamia ya wafuasi wa chama cha
Chadema waliokuwa wakiandamana hadi afisi za tume ya uchaguzi.
Wakati
huo huo mtandao wa wanafunzi Tanzania (TSNP), wamemtaka waziri wa mambo
ya ndani, Mwigulu Nchemba kujiuzulu kutokana na tukio la kuuawa kwa
mwanafunzi wa Akwilina Akwilini.
Taaria zaidi pia zinasema kuwa
polisi 6 wamekamatwa kwa tuhuma za kutumia risasi za moto wakati wa
uchaguzi mdogo mjini Dar es Salaam.
BBC SWAHILI
0 comments: