Mbunge wa Kigoma mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo amefunguka na
kuwataka watu wasirudishwe nyuma kwa vitisho na usumbufu wa sheria
kandamizi zinazopelekea baadhi ya viongozi kukamatwa na kuwekwa ndani.
Zitto Kabwe ameweka wazi hayo mara baada ya kuachiwa leo Februari 23,
2018 na kusema kuwa yeye anaendelea na harakati zake ya kuwafikia
viongozi na Kata ambazo wananchi waliwachagua viongozi wa ACT Wazalendo.
"Tusirudishwe nyuma na vitisho, usumbufu na sheria kandamizi. Harakati
za kulinda Demokrasia yetu na Uhuru wa kukusanyika, kujieleza na
kupashana habari lazima ziendelee. Ni wajibu wetu kulinda Demokrasia ya
Vyama vingi na kuiimarisha iwe madhubuti kwa ajili ya Maendeleo ya Watu
wetu. Baada ya kulala bure jana polisi Morogoro, tunaendelea na kazi
yetu ya kutembelea kata zote ambazo Wananchi walitupa dhamana kwa
kuchagua madiwani wa Act Wazalendo" alisema Zitto Kabwe
Aidha Zitto Kabwe ameonyesha kuguswa na muaji mengine ambayo yametokea
jana ambapo diwani wa CHADEMA ameauwa kwa kukatwa mapanga sehemu
mbalimbali katika mwili wake
"Nawapa pole Wananchi wa Ifakara kwa msiba wa Diwani wao aliyekatwa
mapanga mpaka kufa jana Usiku. Nilipata taarifa hizo nikiwa selo ya
Polisi. Mauaji ya namna hii kwa Viongozi wa kisiasa yanatia doa nchi
yetu na ni mwendelezo ya uvunjifu mkubwa wa haki za raia" alisema Zitto
Kabwe
0 comments: