Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
amewatunuku kamisheni maofisa wanafunzi 197 wa Jeshi la Wananchi wa
Tanzania (JWTZ).
Sherehe hizo zimefanyika leo Februari 3, 2018 katika viwanja vya Ikulu
jijini Dar es salaam, ambapo maofisa hao wapya ni wa Tanzania na kutoka
nchi marafiki, waliopata mafunzo katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi
Monduli mkoani Arusha.
Katia tukio hilo ambalo lilipambwa na magwaride kutoka kwa Wanajeshi hao, lilihudhuriwa na viongozi mbali mbali wa Kitaifa.
Miongoni mwa waliotunukiwa kamisheni hizo wanawake ni 28, na waliobaki ni wanaume.
0 comments: