Kaskazini mashariki mwa Misri
unapatikana mji wa Port Said. Mji wa Port Said una ukubwa wa kilometa 30
tu sawa na mile 19. Una idadi ya wa watu wasiopungua laki sita. Mji huu
ulianzishwa mwaka 1859 wakati wa ujenzi wa mfereji wa Suez. Miaka 61
baada ya kuanzishwa Port Said mwaka 1920 klabu ya Al Masry ilianzishwa.
Klabu ya Al Masry inatumia uwanja wa Al Masry club stadium unaobeba
mashabiki 17,000. Uwanja huu inasadikia ulisababisha kusimamishwa kwa
ligi kuu Misri mwaka 2012 baada ya vurugu kutokea.
Klabu ya Al Masry inakutana uso kwa uso na klabu ya Simba katika
kombe shirikisho. Klabu ya Simba imeweka makazi yake mashariki mwa
Tanzania katika jiji la Dar es salaam. Simba ilianzishwa miaka 16 baada
ya Al Masry kuanzishwa mnamo mwaka 1936. Jiji la Dar Es salaam pia lipo
kwenye ukanda wa pwani kama ililivyo kwa jiji la Port Said ambapo
klabu ya Al Masry inapatikana. Jiji la Dar es salaam hapo awali
lilijulikana kama Mzizima yaani mji wa afya njema kutokana na hali nzuri
ya vyakula hasa hasa shughuli ya uvuvi wa samaki.
Sultan Majid bin said aliamua kutengeneza mji wake ndani ya Mzizima akauita nyumba ya
aman yaani Dar (Nyumba) Es saalam (Amani). Kumbe Dar es salam maana yake
nyumba ya amani ambapo kinyume chake ni Dar al hard yaan nyumba ya
vita. Hapa majiji mawili yanakutana Jiji La Porto lenye vitimbi vya
migogoro hasa katika mfereji wa Suez, pamoja na Vurugu za uwanja wa Port
Said na jiji la Dar Es Salaam linalosifika kwa utulivu na aman.
Klabu ya Al Masry inaongozwa na kocha mkuu Hossan Hassan ambaye pia
aliwahi kuwa mchezaji nguli wa zamani wa taifa la Misri. Hossan Hassan
alizaliwa mwaka 1966 katika jiji la Cairo katika eneo la Helwan ambalo
rais wa zamani wa Misri Gamal Abdel Nasser alitangaza eneo hilo kuwa mji
wa viwanda. Hossan Hassan ndiye mfungaji bora wa muda wote wa timu
taifa ya Misri akiwa na magoli 69 kwenye michezo 169. Anatajwa kama
mchezaji bora katika historia ya soka barani Afrika. Anakumbukwa sana
kule nchini Uswisi kwa kuitandika klabu ya Celtic magoli manne kwenye
mchezo mmoja akiwa na klabu ya Neuchatel Xamax kwenye michuano ya kombe
la UEFA.
Pia aliwahi kuichezea klabu hiyo Al Masry kunako mwaka 2004 mpaka
2006. Mnamo mwaka 2008 alipewa kandarasi ya kuionoa klabu hiyo.
Alitundika daruga akiwa na miaka 42.
Awali ya yote ni watoe hofu mashabiki wa Simba ambao wanadhani Al Masry ni
klabu kubwa kama akina Al Ahly au Zamalek. Klabu hii haijawahi kutwaa
ubingwa ligi kuu Misri tokea ligi hiyo ianzishwe mwaka 1948. ila
imejitahidi kumaliza nafasi tatu za juu kwenye msimamao wa ligi mara
sita tu. Licha ya kuwa haina mafanikio makubwa sana ligi kuu lakini ni
klabu yenye mashabiki wengi sana nyuma ya al Ahly, Zamalek na Ismalia.
Ilikuwa na mafanikio makubwa sana miaka ya 1921 mpaka 1989. Imetwaa
kombe la sultan mara 3, kombe la Misri mara moja mwaka 1998, na kombe la
shirikisho la Misri mara moja nayo ni mwaka 1992.
Pia imetwaa kombe la kanda ya mfereji wa Suez mara 17 kombe ambalo
kwa sasa halipo tena na lilikuwa likijumuisha timu za majiji matatu tu.
Kikubwa Heshima kubwa walio nayo ni kuwa imekosa kushiriki ligi kuu
miaka miwili tu, walishuka daraja mwaka 1957 mpka 1959 baada ya mgogoro
mkubwa kwenye mfereji wa Suez ambapo mapato ya klabu yalishuka na baadhi
ya wachezaji kuondoka. Kiwango chao msimu huu sio cha kutisha sana kama
cha kama moto walio nao vijana wa Manara. Kwanza wapo nafasi ya 4
kwenye msimamo wao wa ligi wakiwa na alama 42 baada ya michezo 23.
Katika michezo kumi ya mwisho ya ligi wameshinda michezo mitano wametoka
suluhu michezo mitatu na wamepoteza miwili.
Nitoe tahadhari, hawa jamaa nao wana balaa lao, wanagawa vipigo kwa timu kubwa na vya
magoli mengi. Mnamo tarehe 5 mwezi wa pili walitoa dozi ya magoli manne
ugenini kwa klabu ya El Maqasa, wakaliza El Tanta magol sita kwa mbili,
wakaizibua El Nasri ugenini kwa magoli matatu kwa mawili. Pia
wakaitandika Zamalek ugenini goli moja.
Katika klabu hii wachezaji wa kuogopwa ni A Bance mwenye mabao matano
akiwa na umri miaka 33, pamoja na mshambuliaji Ahmed Gomaa mwenye
magoli 11 akiwa na umri wa miaka 29, Ahmed Sokri kiungo machachari na
mkongwe mwenye magoli matano akiwa na umri wa miaka 30, mwingine ni
pamoja na Islam Abou Slemma mwenye magoli matano. Ni hayo tu.
0 comments: