Mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma.
WAKATI Donald Ngoma na Kelvin Yondani wakirejea katika kikosi cha Yanga,
timu hiyo kesho inaondoka kwenda Shelisheli tayari kwa kurudiana na St
Louis ikitarajia kuacha wachezaji kumi katika safari hiyo.
Ngoma alianza mazoezi jana asubuhi huku Yondani akithibitishiwa na daktari wa timu hiyo, Edward Bavu kuwa yupo tayari kucheza mechi hiyo ya marudiano itakayochezwa Jumanne ijayo mjini Viktoria, Shelisheli.
Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Jumamosi, msafara wa Yanga utakuwa na wachezaji 20 kati ya 30 ambao imewasajili kwenye msimu huu.
Wachezaji watatu Buruhani Akilimali, Anthony Matheo na kiungo kinda, Maka Edward wao hawatakuwepo katika msafara kwani majina yao hayapo kwenye usajili wa Caf.
Mtoa taarifa wetu alisema, Thabani Kamusoko naye yupo kwenye hatihati ya kuwepo kwenye orodha ya watakaoondoka kutokana na kutokuwa fiti kwa asilimia 100 kucheza mchezo huo.
“Wachezaji watakaobaki ni Amissi Tambwe, Ninja (Abdallah Shaibu), Yohana Nkomola na Ngoma, wengine ni Maka, Matheo na (Burhan) Akilimali ambao majina yao hayakupelekwa Caf.
Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh yeye alisema: “Tumebakisha siku moja kwa ajili ya kufanya mazoezi ambayo ni kesho (leo) halafu tutakuwa na kikosi kamili.
“Ila Ngoma, Tambwe na Ninja hawaendi.”

0 comments: