Mzee
Kingunge Ngombale Mwiru alikuwa akipatiwa matibabu hospitalini hapo
baada ya kushambuliwa na mbwa wake nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam
tarehe 22 Desemba, 2017.
Mhe.
Rais Magufuli amesema Taifa limempoteza mtu muhimu ambaye alitoa
mchango mkubwa katika juhudi za kupigania uhuru na baada ya kupata uhuru
akiwa mtumishi mtiifu wa Chama cha TANU na baadaye Chama Cha Mapinduzi
(CCM), na katika nyadhifa mbalimbali za uongozi ndani ya Serikali.
“Mzee
Kingunge Ngombale Mwiru ametoa mchango mkubwa sana, sisi kama Taifa
hatuwezi kusahau na tutayaenzi mema yote aliyoyafanya wakati wa utumishi
wake uliotukuka, ametuachia somo la kupigania maslahi ya nchi wakati
wote, kuwa wazalendo wa kweli, kudumisha amani na mshikamano, kuchapa
kazi kwa juhudi na maarifa na kuwa na nidhamu” amesema Mhe. Rais Magufuli.
Kufuatia
msiba huu, Mhe. Rais Magufuli amewapa pole wanafamilia wote, wanachama
wa CCM, ndugu, jamaa, marafiki na wote walioguswa na msiba huu, na
amewaombea kuwa na moyo wa subira, uvumilivu na ustahimilivu katika
kipindi hiki cha majonzi.
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu Kingunge Ngombale Mwiru mahali pema peponi, Amina.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
02 Februari, 2018
0 comments: