Tuesday, 10 April 2018

UJUE UMUHIMU WA KUNYWA MAJI MENGI KILA SIKU


Unashauriwa kunywa maji zaidi lita 2 hadi 5 kila siku ili kuepuka mawe kutengenezeka kwenye figo zako. Maji ndio husafisha seli na kuondoa sumu na kemikali zinazojitengeneza mwilini kuwa mawe.

Wanawake ndio waathirika wakubwa wa tatizo hili maana miili yao ina joto kubwa hivyo maji hukaushwa kwenye figo na mawe haya hutengenezeka kirahisi wasipokunywa maji ya kutosha.

Magonjwa ya figo yanakadiriwa kuwaathiri takribani wanawake milioni 195 duniani kote na yanashika nafasi ya 8 kama chanzo cha vifo vya wanawake duniani.

Inakadiriwa kuwa wanawake 600,000 hupoteza maisha kutokana na matatizo ya figo duniani kote kila mwaka.

Nakutakia mazingatio katika hili
Share kwa wote uwapendao...

Friday, 23 March 2018

Ifahamu Afya yako kupitia Rangi ya Mkojo wako
Je unafahamu ya kwamba rangi ya mkoja inakupa matokea sahihi kuhusu  afya yako? Kama jibu ni hapana basi makala haya yanakusu wewe, kwani rangi ya mkoja kwa mujibu wa watalamu wa afya unauwezo mkubwa wa kukuoa ukweli juu ya afya yako.

1. Mweupe kabisa (Usio na Rangi):
Unakunywa maji mengi.

2. Manjano iliyochanganyika na Kijani kidogo. Ni kawaida, una afya na Mwili wako una maji ya kutosha.

3. Manjano iliyo pauka.Upo kawaida tu. Endelea kunywa maji ya kutosha

4. Njano iliyo kolea. Upo kawaida lakini unashauriwa kunywa maji ya kutosha.

5. Njano inayokaribia kufanana na Kahawia au Rangi kama ya Asali. Mwili wako hauna maji ya kutosha. Kunywa maji kwa wingi sasa.

6. Rangi ya Kahawia. Huwenda una Matatizo kwenye Ini lako au Upungufu mkubwa wa Maji mwilini. Kunywa maji ya kutosha na umwone daktari kamali hii ikiendelea.

7. Rangi ya Pinki inayokaribia kuwa kama Nyekundu. Kama hujala matunda yoyote yenye asili ya uwekundu, basi huwenda una famu kwenye kibofu chako cha mkojo. Inaweza ikawa sio ishara mbaya. Lakini inaweza ikawa ishara ya ugojwa wa Figo, uvimbe, matatizo kwenye njia ya mkojo, au matatizo kwenye kibofu. Muone daktari haraka iwezekanavyo.


Friday, 12 January 2018

Lijue Tatizo la Shinikizo la Damu, CHANZO na TIBA YAKE.
Nini maana ya shinikizo la damu?
Ni msukumo wa damu ulio juu kuliko inavyotakiwa kwa muda mrefu. Msukumo wa damu huhitajika mwilini ili kusambaza chakula, oksijeni na kutoa uchafu.

Shinikizo la damu hupimwa kwa kutumia kifaa kinachoitwa Sphygmomanometer

Shinikizo la damu husababishwa na nini?

Vitu vifuatavyo vinaweza kusababisha shinikizo la juu la damu:

    Uvutaji sigara
    Unene na uzito kupita kiasi
    Unywaji wa pombe
    Upungufu wa madini ya potassium
    Upungufu wa vitamin D
    Umri mkubwa
    Ongezeko la kemikali kwenye figo (renin)
    Kushindwa kufanyakazi kwa kichocheo kiitwacho insulin



Uanishaji wa shinikizo la damu

    Presha ya kawaida <120 <80
    Presha inayoelekea kupanda 120-139 80-89
    Presha hatua ya 1 140-159 90-99
    Presha hatua ya 2 160-179 100-109
    Presha hatua ya 3 ≥180 ≥110



Shinikizo la damu/BP ni ugonjwa unaosumbuwa watu wengi sana duniani na hii ni kutokana na kutokujuwa ni nini hasa husababisha ugonjwa huu mwilini. Shinikizo la damu linaonekana kuwa ni ugonjwa wa kuishi kwa kufuata masharti.

Katika makala hii tutaona uhusiano mkubwa uliopo kati ya upungufu wa maji mwilini na ugonjwa huu, mwishoni utakuwa umeelewa sasa ni jinsi gani ilivyo rahisi kabisa kujiepusha na kujiponya ugonjwa huu. Endelea kusoma.

Takwimu za Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) zinasema tayari watu bilioni moja duniani kote, wanaathiriwa na shinikizo la juu la damu huku likisababisha mshtuko wa moyo (Heart Attacks), kupooza na kiharusi (Strokes).

Takribani watu milioni nane hufa kila mwaka kutokana na ugonjwa huu wa kupanda kwa shinikizo la damu.

Dalili za shinikizo la damu:

    Maumivu ya kichwa (Haswa nyuma ya kichwa mara nyingi nyakati za asubuhi),
    Kuchanganyikiwa,
    Kizunguzungu,
    Kelele sikioni (Mvumo au Mazomeo masikioni),
    Kutoweza kuona vizuri au
    Matukio ya kuzirai.
    Uchovu/kujisikia kuchokachoka
    Mapigo ya moyo kwenda haraka
    Kutokuweza kuona vizuri
    Damu kutoka puani
    Uonapo dalili hizi unapaswa kuwahi hospitali kupata vipimo.



‘Mwili wa binadamu unapopungukiwa maji hutoa ishara (indicators), tumeziita ishara hizo kuwa ni magonjwa, hauumwi, una kiu, usiitibu kiu na madawa – dr. Batmanghelidj’.

Shinikizo la damu (hasa la juu) ni kiashiria cha mwili kupungukiwa maji kwa kiwango kikubwa, ni wakati ambapo mwili unajaribu kujizoesha na upungufu wa jumla wa maji wakati kunapokuwa hakuna maji ya kutosha kuijaza mishipa ya damu yenye kazi ya kusambaza maji kwenye seli mhimu.

Mishipa ya damu imebuniwa maalumu kuendana na mtiririko uliosawa wa ujazo wake wa damu na mahitaji mbalimbali ya tishu kwa kufunga na kufungua mishipa mbalimbali ya damu ndani ya mwili.

Figo hushtuka upesi kulingana na mtiririko wa damu. Hili linaposhindikana, yaani iwapo mtiririko au ujazo wa damu utapungua, basi Figo huitoa homoni iitwayo ‘renini’ ambayo yenyewe huzarisha kitu kiitwacho ‘angiotensini’ ambayo huwa na matokeo mawili; kwanza huzibana ateri na kupandisha shinikizo la damu, pili huisababisha tezi ya ‘adreno’ kutoa homoni iitwayo ‘aldosteroni’ ambayo huzifanya figo kuishikilia chumvi na hivyo kusababisha kupanda kwa shinikizo la damu.

Asilimia 94 ya damu ni maji. Kwa ujumla kila seli ndani ya miili yetu ina bahari ya maji baridi ndani yake na bahari ya maji chumvi nje yake. Afya bora inategemea uwiano mzuri wa maji ya bahari hizo mbili.

Chumvi inayashikilia na kuyalazimisha baadhi ya maji kubaki nje ya seli (osmotic retention) na potasiamu inayashikilia maji ndani ya seli.

Wakati mwili unapokuwa katika upungufu wa maji (yaani haunywi maji ya kutosha kila siku) mwili utaongeza ujazo wa maji chumvi kwenye bahari ya nje ya seli.

Kupitia mfumo maalumu, homoni iitwayo ‘vasopressini’ hutolewa ambayo inaweza kuyachuja maji ya chumvi toka katika bahari ya nje ya seli na kuyachoma maji hayo baridi (baada ya kuwa yamechujwa) ndani katikati ya bahari ya ndani ya seli kama yanavyohitajika ili kuutunza uwiano sawa wa maji ndani na nje ya seli.

Lakini ili mbinu hii ifanikiwe, mbinu gani, mbinu ya kuyachuja maji ya chumvi toka katika bahari ya nje ya seli, vasopressini husababisha kapilari na mishipa ya damu kujikaza au kupunguza vipenyo vyake na kukupatia wewe shinikizo la juu la damu (BP) ambalo ni mhimu ili kuyachuja na kuyachoma maji baridi ndani ya seli toka katika bahari ya maji chumvi iliyopo nje ya seli.

Kama mishipa ya damu haitapunguza vipenyo vyake, baadhi ya gesi itaachana na damu ili kuziba nafasi zilizowazi kutokana na kupungua kwa umajimaji mwilini na hatimaye kukusababishia msongamano wa Gesi (Gas locks).

Sifa hii ya vipenyo vya mishipa ya damu kujirekebisha kwa ajili ya mzunguko wa damu, ndiyo mtindo unaotumika zaidi katika kanuni za kihaidroliki wakati ambapo mzunguko wa damu mwilini umejirekebisha kuendana na kiasi cha umajimaji kinachopatikana.

Wakati mwili unapokuwa katika upungufu wa maji kwa mfano kutokana na kutokunywa maji ya kutosha; asilimia 66 ya kuishiwa maji inajionesha kwa kupungua kwa ujazo wa seli, asilimia 26 inapotea toka ujazo wa umajimaji uliopo sehemu ya nje ya seli na asilimia 8 tu inapotea toka katika ujazo wa damu.

Shinikizo la juu la damu ni kiashirio cha mwili kupungukiwa maji kwa asilimia 8 tu, lakini madhara yanajitokeza sababu ya asilimia 66 ya kupunguwa kwa ujazo wa seli.

Maji na chumvi vitalirudisha shinikizo la damu katika hali yake ya kawaida.

Hii ndiyo sababu shinikizo la damu linapaswa kutibiwa kwa kuongeza unywaji wa maji pekee. Dr.Batmanghelidj anasema; Maji peke yake, ni dawa bora ya kukojosha, pekee ya asili tuwezayo kuiendea.

Kama watu wanaosumbuliwa na shinikizo la damu wangeongeza kiasi cha uchukuaji maji, hawatazihitaji dawa za kukojosha, watazarisha mkojo wa kutosha na hivyo kuiondoa chumvi iliyokuwa imezidi!. Watatakiwa pia kuacha kula vyakula visivyo na chumvi na hivyo kuepukana na mikakamao ya mishipa (cramps) kwenye miguu yao.

Madhara yanayoweza kuletwa na shinikizo la damu:
Kwa mjibu wa dr.Batmanghelidj, kutokulielewa shinikizo la damu kama moja ya ishara za mwili kupungukiwa maji na kulitibu kwa dawa za kukojosha ambazo zinaukausha mwili zaidi, baada ya muda zitasababisha;

    Kuzibika kwa ateri za moyo na ateri ziendazo kwenye ubongo
    Shambulio la moyo (heart attack)
    Mishtuko midogo midogo au mikubwa inayopelekea kuzimia
    Ugonjwa wa kibofu cha mkojo
    Kiharusi
    Kupungua kwa nguvu za kiume kwa upande wa wanaume
    Kuharibiwa kwa ubongo na matatizo ya akili kama vile kupoteza kumbukumbu (Alzheimer).

Daktari mwingine, Dr.David Brownstein katika kitabu chake kiitwacho; “Salt Your Way to Live”, anasema kwamba alifundishwa katika vyuo vya kiganga kuwa chumvi husababisha shinikizo la damu na kuwa kila mmoja lazima ale vyakula vyenye chumvi kidogo. Na hili watu wengi wamekuwa wakiamini hivi.

Wakati akiwatibu wagonjwa wake, anasema; alianza kuona kuwa wale wanaotumia vyakula vyenye chumvi kidogo wanapata matokeo ya chini au wanapata nafuu ndogo sana kutoka katika vyakula hivyo vyenye chumvi kidogo au bila chumvi kabisa na wengi wao walitokewa kuwa na uhaba mkubwa wa madini katika miili yao.

Katika utafiti wake ili kuwasaidia wagonjwa wake, ndipo akaja na jibu la chumvi ya baharini ambayo haijasafishwa (unrefined sea salt) ambayo huwa na madini mengine zaidi ya 80 ndani yake, alianza kuona kitu kigeni kinaanza kutokea. Wagonjwa wake hao wakaanza kuona mashinikizo yao ya damu yanaanza kushuka katika kiwango ambacho wanaweza kuachana kabisa na matumizi ya dawa.

Dr.Batmanghelidj anasema, ikiwa watu watajishughulisha na mazoezi hasa mazoezi ya kutembea kwa miguu, watakunywa maji halisi zaidi na kuongeza chumvi (siyo sodiamu) kidogo ya ziada kwenye vyakula vyao, mashinikizo yao ya damu yatarudi katika hali yake ya kawaida.

Swali la kujiuliza; Ni zaidi ya miongo minne sasa tangu tulipoambiwa kula vyakula vyenye chumvi kidogo ili kuepukana na shinikizo la damu, kwanini sasa Idadi ya watu wanaopatwa na ugonjwa huu inazidi kuongezeka?.

Narudia tena, mwili unapoanza kuishikilia chumvi, hufanya hivyo ili kuhifadhi maji, toka katika bahari chumvi hiyo ya nje ya seli, maji huchujwa na kutumika wakati wa mahitaji ya dharura.

Maji na chumvi kwa pamoja vitalirudisha shinikizo la damu katika hali yake ya kawaida. Kuikimbia chumvi kunasababisha shinikizo la damu (BP) kuwa sehemu ya maisha yetu, tutapata nafuu, lakini baada ya muda mfupi hali hurudi ileile na pengine kuwa watumwa wa kuchagua kula hiki au kile.

Tofauti na zamani ambapo shinikizo la juu la damu lilipokuwa ni ugonjwa wa watu wanene au wenye uzito uliozidi pekee, siku hizi wanene kwa wembamba, watoto kwa wakubwa wanaugua BP.

Mambo 11 mhimu ya kuzingatia unapokuwa na shinikizo la juu la damu:

    Ongeza kiasi cha unywaji maji na chumvi kila siku
    Kula nyama isiyo na mafuta mengi
    Ongeza kula vyakula visivyokobolewa
    Kula zaidi matunda, mboga za majani, karanga na maharage
    Punguza vyakula vya viwandani vinavyoongezwa sukari nyingi
    Punguza vyakula vyenye lehemu au kolesteroli nyingi
    Acha kuvuta sigara na tumbaku za aina zote
    Acha kunywa pombe
    Dhibiti uzito wako, hakikisha una uzito unaopaswa kuwa nao kwa mjibu wa urefu wako
    Punguza mfadhaiko au stress
    Fanya mazoezi ya viungo hasa mazoezi ya kukimbia kila siku na kama kukimbia kimbia huwezi basi kutembea kwa miguu masaa mawili kwa siku inatosha kabisa.
Zijue Njia za Kupata Ujauzito kwa Haraka Kwa Mwanamke
    Kufanya tendo la ndoa mara kwa mara, angalau siku tatu kwa wiki, ikiwezekana on alternate days.
    Tumia ovulation prediction kit, hiki ni kifaa ambacho kitakusaidia kujua wakati hasa mwanamke ameengua yai na ndio kipindi ambacho mwanamke ana uwezo wa kushika mimba akikutana na mumewe. Ni rahisi kutumia.
    Fanya tendo la ndoa kabla ya kuengua yai (kabla ya ovulation), huongeza uwezekano wa kushika mimba kuliko kusubiria ovulation au kufanya baada ya ovulation. Kutaneni siku mbili au tatu kabla ya ovulation. Ukitumia ovulation test kit, mkutane kuanzia siku itakapokuwa positive kwani huwa inapredict ovulation kutokea 48 hrs after it tests positive.
    Usitegemee njia ya kalenda kutabiri uenguaji yai, njia hii kwa kiasi fulani huweza kuwasaidia wale wenye mzunguko wa siku 28, lakini pia haina uhakika wa 100%, wengi wa wanawake hawaengui yai siku ya 14 ya mzunguko wa hedhi, kwa hiyo kutegemea kalenda kutakuchelewesha kupata ujauzito.
    Unapotaka kushika mimba, acha au punguza kwa kiasi kikubwa matumizi ya pombe, sigara au dawa za kulevya.
    Unapotaka kupata mimba, tendo la ndoa liwe kitu 'enjoyable' na sio tendo 'mechanical' kwa ajili ya kutafuta mtoto. Plan a romantic evening or try something different to spice things up. How you are feeling sexually may increase your chances of getting pregnancy. For women a better orgasm may help pull the sperms into the uterus and for men a better orgasm may increase their sperm count.
    Kufanya mapenzi katika mtindo (style) ambayo itafanya mbegu za kiume zikae kwa muda mrefu ukeni na hivyo nyingi kupanda kuingia kwenye kizazi na kwenda kurutubisha yai. 'missionary position' ni nzuri zaidi, ambapo mwanaume anakuwa juu, epuka positions za mwanamke kuwa juu kwani hufanya mbegu zimwagike kwa gravity. Jaribu pia kuweka mto chini ya kiuno ili kukiinua na kufanya mbegu ziingie ndani kwa urahisi zaidi.


Kumbuka kuna asilimia 10 - 25 ya couples ambazo zina matatizo ya infertility lakini vipimo havionyeshi tatizo, inaweza kuwa namna ya kufanya mapenzi ndio ikawa shida, jaribu njia hizo 7 juu.

Thursday, 11 January 2018

Jinsi Punyeto Inavyo Sababisha Ukosefu Na Upungufu Wa Nguvu za Kiume
Ukosefu  na/ama  upungufu  wa  nguvu  za  kiume, ni  tatizo  linalo  wakabili  mamilioni  ya  wanaume  duniani.  Zipo  sababu  nyingi  zinazo  sababisha  tatizo  la  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume. 

Miongoni  mwa  sababu  hizo  ni  pamoja  na  maradhi  kisukari, presha,shinikizo  la  damu, moyo, figo, matatizo  kwenye  mishipa  ya  ubongo  &  mishipa  ya  uti  wa mgongo, matatizo  kwenye  mishipa itumikayo  kusafrisha damu  mwilini, maradhi  ya  ngiri,  pamoja  na   upigaji  punyeto  kwa  muda  mrefu.


Katika  makala  yetu  ya  leo, tutaangalia  namna   suala  la  upigaji  punyeto linavyo  athiri  nguvu  za  kiume.

Kabla  hatujaangalia  namna  suala la upigaji  punyeto linavyo  maliza  nguvu  za  kiume, ni  vyema  tukafahamu  kwanza  kuhusu  SAYANSI  YA  MFUMO  WA  NGUVU  ZA  KIUME.


Kufahamu   kuhusu   SAYANSI  YA  MFUMO  WA  NGUVU  ZA  KIUME .
Ukisoma  vizuri  kuhusu  mfumo  wa  nguvu  za  kiume, utagundua  kuwa   Suala  la  nguvu  za  kiume  ni  suala  la  kimfumo.  Ili  mwanaume  awe na nguvu  za  kiume, aendelee  kuwa  na  nguvu  za  kiume na  azilinde  nguvu  zake za  kiume, ni  lazima  ogani  zote zinazo  husika  na  mfumo  wa  nguvu  za  kiume  ziwe  na  afya  njema  na  ziwe  na  ushirikiano   thabiti  na  wenye  afya.

Vile  vile , utagundua  kuwa , mambo  makuu  muhimu  katika   mfumo  wa  nguvu  za  kiume  ni  kama  ifuatavyo:

i.Mishipa  imara  ya  ubongo  na  yenye  afya  njema

ii. Mishipa  imara  ya  uti  wa  mgongo  (  spinal  cords )

iii.Mishipa  imara  itumikayo  kusafirisha  damu  mwilini  (  Blood Vessels )

iv. Mfumo  imara  wa  usafirishaji  damu  mwilini

v. Mishipa  ya  uume  iliyo  imara  na  yenye  afya  njema

vi. Uhusiano  imara  na  wenye  afya  kati  ya  mishipa  ya  fahamu  iliyopo  katika  ubongo, mishipa  ya  kwenye  uti  wa  mgongo  pamoja  na  misuli & mishipa  ya  kwenye  uume.

Hivyo  basi, ili  mwanaume  aweze  kuwa  na  nguvu  imara  za  kiume, na  aendelee  kuwa  na  nguvu  hizo ni  lazima  mambo  yote  muhimu  katika  mfumo  wa  nguvu za  kiume  yawe  imara  pasi na  hitilafu  yoyote.

Hitilafu  yoyote  katika  mambo  hayo, itasababisha  ukosefu na/ama  upungufu wa  nguvu  za  kiume  kwa  mwanaume  huyo.  Pale inapotokea    hitilafu  ama  mapungufu  katika  ogani  zaidi  ya  moja  kati  ya  zilizo  tajwa hapo  juu, basi  tatizo  kwa  muhusika  huwa  kubwa  mara  dufu.

JINSI  PUNYETO  INAVYO  SABABISHA  TATIZO  LA  UKOSEFU &  UPUNGUFU  WA  NGUVU  ZA  KIUME.
Mwanaume   anapopatwa na  wazo  la  kufanya  tendo  la  ndoa, ubongo  hutoa  ishara  kwenye  mishipa  ya  uti  wa  mgongo  ambayo  nayo  husafirisha  taarifa  hadi  kwenye  mishipa &  misuli  ya  uume.

Mishipa  ya  uume inapopokea  taarifa  hiyo, hutanuka. Na  mishipa  ya  uume  inapotanuka, hufanya  mambo  mawili  muhimu  sana :

i.Husababisha  mishipa  ya  ateri  kupanuka  na  hivyo  kuruhusu  damu  kuingia kwa  kasi  sana   ndani  ya  mishipa  ya  uume  na  hivyo  kuufanya  uume  usimame  na  kuwa  imara  bara bara.

ii. Huibinya na  kuiziba  mishipa  ya  vena  na  hivyo  kuzuia  kunyonya  ama  kufyonza  damu  iliyo  ingia  ndani  ya  mishipa ya  uume.  (  KAZI  KUBWA  YA  MISHIPA  YA  VENA  ILIYO  KARIBU NA  MISHIPA  YA  UUME  NI KUHAKIKISHA  HAKUNA  DAMU NDANI YA  MISHIPA  YA  UUME. HIVYO  BASI  DAMU  INAPOINGIA  NDANI YA  MISHIPA  YA  UUME, MISHIPA  YA  VENA  HU “SENSE” JAMBO  HILO  KWA  HARAKA  NA HIVYO  KUIFYONZA  DAMU  HIYO  KUTOKA KWENYE MISHIPA  YA UUME  YA  KUITOA  NJE YA MISHIPA  YA  UUME.  NA  DAMU INAPOKOSEKANA  NDANI  YA  MISHIPA  YA  UUME, HUUFANYA  UUME  KUSINYAA  NA  KULEGEA )

Mtu  anayepiga  punyeto  husababisha  mambo  yafuatayo  katika  mwili  wake :

1. Huuwa  nguvu  ya  mishipa  & misuli ya  uume ambayo  ndio  inayo husika  na  kusimama  kwa  uume

2. Mishipa  ya   uume  inapo  sinyaa  na  kukosa  nguvu  yake  ya  asili, husababisha  mambo  yafuatayo :

i.Huondoa  uwezo  wa  mishipa  &  misuli  ya  uume  kutanuka, na  hii  ndio  sababu  inayo  wafanya  waathirika  wa  punyeto  kutumia  nguvu  nyingi  sana  katika  kuufanya  uume  usimame.

ii.Huondoa  uwezo  wa  mishipa &  misuli  ya  uume  kuibana  na  kuiziba  mishipa  ya  vena, na  hii ndio  sababu  inayo  fanya  waathirika  wa  punyeto  kufika  kileleni  haraka  sana, kwani damu  inayo  ingia  kwenye misuli  ya  uume   hufyonzwa  ndani ya  muda  mfupi sana.

 Hii  hutokea  kwa  sababu  mishipa na  misuli  ya  uume inakuwa  imelegea,na  mishipa  ya  vena inakuwa  imepwaya, hivyo  msuguano wowote ule  hufanya  mishipa  ya  vena  kufunguka  na  kufyonza  damu  kutoka  kwenye mishipa  ya  uume  na hivyo  kuufanya  uume  kusinyaa  ndani ya dakika ama sekunde  chache sana.

3. Vile  vile  punyeto  hufanya  uume  kusinyaa na  kurudi ndani  na  kuufanya  uonekane kama  uume  wa  motto mdogo.

Kwa  ufupi  punyeto  husababisha  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume  kwa  sababu  kuu  zifuatazo :

i.Kwanza   hudhoofisha  na  kuharibu  mishipa  ya  uume,  ambayo  ndio  hufanya  uume kusimama.

ii.Pili  hudhoofisha  utendaji  kazi  wa  mishipa  ya  ateri, ambayo  ndio  hutumika  kama  njia  ya  kusafirisha  damu kupeleka kwenye  misuli  ya  uume  na  ivyo  kuufanya  uume  usimame

iii. Tatu, punyeto  hupelekea  kuvuja  kwa  mishipa  ya  vena  na  hivyo  kusababisha  damu  kufyonzwa  kwa  haraka  sana  kila  iingiapo ndani  ya  misuli ya  uume  na  matokeo  yake  ni  uume   kusimama  kwa  muda  mfupi  sana  wakati wa  tendo  la  ndoa.

iv. Punyeto  huathiri  mtiririko  wa  damu  kwenda  kwenye  mishipa  ya  uume, kwa  sababu  hudhoofisha  misuli &  mishipa  ya  uume  pamoja  na mishipa ya  ateri  ambayo  ndio  hutumika  katika  kusafirisha  damu kwenda  kwenye  uume

DALILI  ZA  MTU  ALIYE  ATHIRIWA  NA  PUNYETO
Dalili  kuu  za  mtu  aliye athiriwa  na  punyeto  ni  kama  ifuatavyo:

i.           Uume  kusinyaa  na  kuwa  kama  wa  mtoto
ii.         Uume kurudi  ndani
iii.       Uume  kusimama  ukiwa  legelege
iv.       Kufika  kileleni  haraka  wakati  wa  tendo  la  ndoa.

TIBA   YA   NGUVU  ZA  KIUME  KWA MTU  ALIYE  ATHIRIKA  NA  PUNYETO.
Dawa   asilia  ya  nguvu  za  kiume iitwayo JIKO  ni tiba  bora  na  ya  uhakika  kabisa  kwa  mtu  aliye  athiriwa   na  punyeto.  Dawa  hii, pamoja  na  mambo  mengine  mengi, husaidia  kufanya  mambio  yafuatayo  katika  mwili  wa  mwanaume  aliye  athiriwa  na  punyeto :

i.Kuimarisha  mishipa  & misuli  ya  uume  ulio  legea na  hivyo  kuurejeshea  uwezo wake wa  asili

ii. Hutibu   tatizo  la  uume  kurudi  ndani

iii.Humaliza  tatizo  la  kusimama  kwa  uume  ukiwa  legelege

iv.Hutibu  na  kuponya  kabisa  tatizo  la  kufika  kieleleni  haraka.

BEI  YA  DAWA  :  Dawa  hii  inapatikana  kwa  gharama  ya  SHILINGI  ELFU  THEMANINI  TU (Tsh. 80,000/=)

MAHALI  INAPOPATIKANA :  Dawa  hii  inapatikana  katika  duka  la  dawa  asilia  liitwalo  NEEMA  HERBALIST  &  NUTRITIONAL  FOODS  CLINIC  lililopo  jijini  DAR  ES  SALAAM  katika  eneo  la  UBUNGO   nyuma  ya  jengo  la  UBUNGO  PLAZA   karibu  na SHULE  YA  MSINGI  UBUNGO  NATIONAL  HOUSING.

Kwa  wateja  wasio  weza  kufika  ofisini  kwetu. Watafikishiwa  dawa  mahali  popote  walipo  jijini  DAR  ES  SALAAM.

Kwa   wateja  waliopo  mikoani  watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  MABASI

Kwa  wateja  waliopo   Zanzibar  wata fikishiwa  dawa  kwa  njia  ya  usafiri  wa boti.

Na  kwa  wateja  waliopo  UGHAIBUNI  watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  POSTA  ama  DHL.

MAWASILIANO :  WASILIANA  NASI   KWA  SIMU  NAMBA  0766  53  83  84.

Kwa  taarifa  zaidi  kuhusu  huduma  zetu, tutembelee kila  siku  kwenye  blogu  yetu :
Agizo la Waziri wa Afya kuhusu wagonjwa Muhimbili kuhamishwa na kusitishwa kwa rufaa

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu, ameagiza wagonjwa wasiotakiwa kufanyiwa upasuaji waliopo hospitali ya taifa Muhimbili kuhamishiwa hospitali ya Mloganzila.

Waziri Ummy ametoa agizo leo alipotembelea hospitali ya Chuo cha Afya na Sayansi shirikishi Kampasi ya  Mloganzila Jijini Dar es Salaam. Ameeleza lengo kuu la kuhamishwa kwa wagonjwa hao ni kupunguza msongamano katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Ummy ameongeza kuwa Wizara yake imejipanga kuongeza madaktari bingwa kutoka hospitali ya Taifa Muhimbili kwenda kuwahudumia wagonjwa watakao hamishiwa katika hospitali ya Mloganzila.

Pia amezitaka hospitali za Wilaya kama Amana na Mwananyamala kuwapa rufaa wagonjwa wasiohitaji upasuaji ya kwenda Mloganzila.

Kwa Upande wake Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Huduma na Hospitali ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili Kampasi ya Mloganzila, Professa Said Abood, amesema kuwa wamejipanga kuhudumia wagonjwa wote watakao wasili kutoka Muhimbili.

Profesa Abood ametaja Magonjwa yaliyoagizwa kutibiwa hospitalini hapo kuwa ni yale yasiyo hitaji upasuaji kitaalamu yanaitwa Magonjwa ya ndani kama vile Malaria, na mengine. Aidha Abood amesema tayari wameshaanza kuwapokea wagonjwa hao wanaotoka Muhimbili.

Monday, 8 January 2018

ZIJUE DALILI ZA TEZI DUME.
Ugonjwa wa tezi tume imeelezwa ya kwamba ni miongoni mwa magonjwa ambayo yanasumbua jamii yetu kwa kiwango kikubwa sana na hata kupelekea kusababisha vifo.

Hata hivyo tafiti mbalimbali zinazidi kuonesha ya kwamba  wanaume ambao wanatumia pombe kali kwa kiwango kikubwa wapo hatarini kupata ugonjwa huo. Licha ya wanywaji wa pombe kali lakini inasadikika ya kwamba wanaume ambao wanafanya kazi za viwandani, husasani viwanda vya rangi au wanaofanya kazi ya kupaka rangi wapo hatarini kupata  ugonjwa huo.

Lakini pia wanaume ambao wapo hatarini kupata ugonjwa huo ni pamoja na wanaume wenye historia ya tatizo hili wenye familia zao, yaani wale ambao mmoja wa ndugu zake (kaka au mdogo wa kiume) au baba kama amewahi ugua ugonjwa huu.

Lakini pia watalamu mbalimbali wa masuala ya afya, wanazidi kueleza ya kwamba wanaume wenye umri wa kati ya miaka 40-70 wapo hatarini kupata ugonjwa huu wa tezi dumi.

Lakini licha ya kuendelea kusambaa kwa kasi kwa ugonjwa huu watalamu wa afya wanaeleza ya kwamba endapo ugonjwa huu wa tezi tume utaweza kutambulika mapema unaweza kutibika.

Dalili za ugonjwa  wa saratani dume.
Katika hatua zake za awali, dalili za saratani ya tezi dum hazitofautiani na zile za kuvimba kwa tezi dume (BPH). Dalili hizo ni pamoja na

1.    Kukojoa mkojo uliochnanganyika na damu.

2.    Kukojoa mara kwa mara hasa nyakati za usiku.

3.    Kukojoa mkojo wenye mtiririko mchafu.

4.    Kutirirka kwa mkojo baada ya kumaliza kukojoa.

5.    Kupata maamuvu wakati unapoanza kukojoa.

Thursday, 4 January 2018

Lijue Tatizo la Figo Kushindwa Kufanya Kazi (Renal/Kidney Failure)
Figo ni miongoni mwa viungo muhimu sana katika mfumo wa utendaji kazi wa mwili wa binadamu. Kwa kawaida, mwili wa binadamu una figo mbili zenye maumbo yanayofanana kama yale ya maharage, yakiwa yamejificha nje ya utando unaozunguka tumbo, chini kidogo ya mbavu za chini.

Kazi za figo
Kazi kuu za figo ni kuchuja vitu mbalimbali pamoja na sumu kadhaa katika damu na hivyo kusaidia katika kuhifadhi na kuthibiti kiwango cha maji na madini (electrolytes) mwilini. Katika kutekeleza hayo, figo huchuja vitu hivyo pamoja na maji yaliyo mwilini na kutengeneza mkojo, huchuja pia maji yasiyohitajika mwilini huku yakinyonya madini na kemikali muhimu kuzirudisha katika mzunguko wa damu na kutoa nje uchafu usiohitajika.

Kazi nyingine za mafigo ni

    Kurekebisha na kuthibiti kiasi cha vitu mbalimbali katika damu pamoja na kiasi cha maji katika mwili.
    Husaidia kutengeneza kiasili cha erythropoietin ambacho ni muhimu sana katika utengenezaji wa chembe nyekundu za damu.
    Husaidia uzalishaji wa vitamini D
    Husaidia pia katika kuthibiti na kurekebisha shinikizo la damu mwilini (blood pressure)



Utengenezaji wa mkojo
Kwa kawaida damu inayozunguka mwilini hatimaye huingia kwenye figo kwa ajili ya kuchujwa, kutoa uchafu pamoja na sumu nyingine zisizohitajika mwilini. Kitendo hiki cha utengenezaji mkojo hufanyika katika hatua kuu zifuatazo;

Hatua ya kwanza ni uchujaji. Damu kutoka nje huingia ndani ya mafigo na kupita kwenye glomeruli, lenye umbo kama chekeche/chujio ambalo limeundwa na mishipa mingi midogo ya damu iliyojizungusha pamoja. Vitu mbali mbali, maji pamoja na sumu zilizo katika damu inayopita kwenye vimishipa hivi na kisha kuingia katika mirija mingine mikubwa kwa ajili ya uchujaji zaidi.

Mirija inayofuata huendelea kuchuja damu na kunyonya baadhi ya vitu vilivyo chujwa kimakosa kuvirudisha mwilini, mpaka kiasi sahihi cha uchafu kinachotakiwa kuchujwa kinapokuwa kimefikiwa.

Mara baada ya mkojo kutengenezwa na kutolewa kwenye figo, husafiri kuingia kwenye kibofu cha mkojo kwa kupita kwenye mirija ijulikanayo kama ureta. Kutoka kwenye kibofu, mkojo hutolewa nje ya mwili kupitia kwenye mrija waurethra.

Figo kushindwa kufanya kazi (Renal Failure/ Kidney Failure)
Kushindwa kufanya kazi kwa figo hutokea iwapo sehemu ya figo au figo lote litapoteza uwezo wake wa kuchuja maji na uchafu kutoka katika damu na kutengeneza mkojo. Kitendo hiki husababisha kusanyiko la uchafu pamoja na sumu kadhaa katika damu ambazo ni hatari kwa afya ya mhusika.

Aina za figo kushindwa kufanya kazi

    Figo kushindwa kufanya kazi kumeganyika katika makundi yafuatayo
    Figo kushindwa kufanya kazi kwa ghafla (Acute Renal Failure (ARF) au Acute Kidney Failure (AKF).
    Figo kushindwa kufanya kazi kwa kiasi (Mild renal/kidney insufficiency)
    Tatizo sugu la figo kushindwa kufanya kazi (Chronic renal failure)



Figo kushindwa kufanya kazi kwa ghafla (Acute Renal Failure (ARF)
Hii ni hali inayotokea kwa ghafla, na kudumu kwa saa chache mpaka siku chini ya 14, na kusababisha ongezeko la kiwango cha creatinine na urea katika damu. Hali hii huwapata karibu asilimia 5% ya wagonjwa waliolazwa hospitali kwa sababu ya matatizo mbalimbali. Aidha hali hii hutokea zaidi kwa wagonjwa mahututi na wale wanaohitaji uangalizi wa kipekee, yaani waliolazwa ICU.

Katika makala hii tutatumia zaidi kifupisho cha ARF.

Visababishi na aina za ARF
Visababishi (au aina) vya ARF vinaweza kugawanywa katika makundi makuu matatu:
Matatizo yanayoathiri mtiririko wa damu kabla ya kuingia katika figo (Prerenal causes/failure)
Matatizo ndani ya figo lenyewe yanayozuia na kuathiri uchujaji wa damu au uzalishaji wa mkojo (Renal causes/failure)
Matatizo yanayoathiri mtiririko wa mkojo nje ya figo (Postrenal causes/failure)

Matatizo yanayoathiri mtiririko wa damu kabla ya kuingia katika figo (Prerenal

causes/failure)
Aina hii hutokea kwa takribani asilimia 60 mpaka 70 ya ARF zote. Katika kundi hili, figo hukosa damu ya kutosha kwa ajili ya kuchuja na hatimaye hushindwa kufanya kazi yake ipasavyo. Mambo yanayoweza kusababisha prerenal failure ni pamoja na:

Upungufu wa maji mwili unaosababishwa na kutapika kupita kiasi, kuharisha, au kupoteza damu kupita kiasi (kwa sababu ya ajali au kuumia)

Kuvurugika kwa mtiririko wa damu inayoingia kwenye figo kwa sababu ya:

    Kushuka kwa ghafla kwa shinikizo la damu kwa sababu ya kupoteza damu nyingi wakati wa upasuaji mkubwa, kuumia au kuungua sehemu kubwa ya mwili, au maambukizi katika mfumo wa damu (sepsis) yanayoweza kufanya mishipa ya damu kutanuka na kushusha shinikizo la damu
    Kuziba au kusinyaa kwa mishipa inayopeleka damu kwenye figo
    Moyo kushindwa kufanya kazi (heart failure) au shambulio la moyo (heart attack) linalosababisha kushuka kwashinikizo la damu
    Ini kushindwa kufanya kazi (liver failure) kunakoweza kusababisha mabadiliko katika mfumo wa homoni zinazoathiri shinikizo la damu pamoja na mtiririko wa damu kwenda kwenye figo.



Mwanzoni kabisa mwa pre-renal failure huwa hakuna athari yoyote inayotokea kwenye figo, na mara nyingi, figo laweza kurudi katika hali yake ya kawaida iwapo chanzo cha tatizo kitagunduliwa na kushughulikiwa ipasavyo.

Matatizo ndani ya figo lenyewe yanayozuia na kuathiri uchujaji wa damu au uzalishaji wa mkojo (Renal causes/failure)

Mambo yanayosababisha madhara katika figo husababaisha karibu asilimia 25 mpaka 40 ya vyanzo vyote vya ARF. Visababishi vilivyo katika kundi hili hujumuisha vile vinavyoathiri uchujaji, mtiririko wa damu ndani ya figo na seli za figo zinazoshughulika na uchujaji na ufyonzaji wa chumvi na maji.

Visababishi hivyo ni pamoja na:

    Magonjwa katika mishipa ya damu
    Kuwepo kwa damu iliyoganda ndani ya mishipa ya damu inayopita katika figo
    Ajali/Kuharibika kwa tishu na seli za figo
    Magonjwa ya mzio katika glomeruli na figo kwa ujumla (glomerulonephritis). Magonjwa yanayoweza kusababisha hali hii ni pamoja na maambukizi (infection) ya bacteria jamii ya streptococci.
    Magonjwa ya mzio katika nyama za figo (acute interstitial nepthritis). Mambo yanayoweza kusababisha hali hii ni pamoja na matumizi ya baadhi ya madawa kama vile Aspirin, Ibuprofen (Brufen), baadhi ya antibiotics, na baadhi ya dawa za kutoa maji mwilini (antidiuretics); magonjwa kama vile saratani ya damu (leukemia), lupus na lymphoma. Magonjwa ya mzio katika nyama za figo husababisha madhara katika seli zinazohusika na uchujaji na ufynzaji wa chumvi na maji.
    Magonjwa ya ukosefu wa damu katika mirija ya figo (acute tubular necrosis) ambayo hufanya seli na tishu za mirija hii kufa na hivyo mirija kushindwa kufyonza chumvi na maji kuyarudisha mwilini. Mambo yanayosababisha hali hii ni pamoja na shock (upungufu wa damu kuingia kwenye figo), matumizi ya madawa kama vile baadhi ya antibiotiki, sumu, dawa zinazotumika viwandani na kwenye x-rays na baadhi ya madawa yanayotumika kutibu saratani.



Matatizo yanayoathiri mtiririko wa mkojo nje ya figo (Postrenal causes/failure)
Mambo yanayosababisha hali hii huchangia kati ya silimia 5 mpaka 10 ya vyanzo vyote vya ARF. Postrenal failure wakati mwingine huitwa pia obstructive renal failure kwa sababu husababishwa na mambo yanayozuia utoaji wa mkojo nje ya figo.

Kuziba kwa ureta moja ama zote mbili kunaweza kusababishwa na:
Vijiwe figo (renal stones)
Saratani ya viungo vya njia ya mkojo au viungo vilivyo karibu na njia ya mkojo kiasi cha kuzuia mkojo kutoka nje ya figo
Matumizi ya baadhi ya madawa

Kuziba kwa njia ya mkojo katika eneo la kibofu cha mkojo kunaweza kutokana na:

    Kijiwe kibofu (bladder stone)
    Kuvimba kwa tezi dume (hii ni kwa wanaume)
    Kuwepo kwa damu iliyoganda katika kibofu
    Saratani ya kibofu cha mkojo
    Matatizo ya mfumo wa fahamu yanayoathiri utendaji kazi wa kibofu cha mkojo



Tafsiri nyingine ya ARF
Wagonjwa wa ARF wanaweza kupata mkojo kidogo sana au wasipate kabisa., au wanaweza kuwa na ongezeko la creatinine kwa kasi ya kutisha au kwa kasi ndogo sana. Hali hizi zinaweza pia kutumika kutoa tafsiri nyingine ya maana ya ARF.

Mtu anayetoa kiasi cha mkojo chini ya 400mL kwa siku hujulikana kama ana oliguria, na huchukuliwa kuwa ana hali mbaya ya kutoweza kupona.

Mtu anayetoa mkojo chini ya 100mLkwa siku husemwa ana Anuria, ambayo kama imetokea ghafla, huashiria kuwepo kwa tatizo la kuziba kwa mirija inayotoa mkojo kwenye figo zote mbili, na mara niyingi hali hii ni ya hatari zaidi. Tafsiri hii husaidia sana katika kuamua aina ya matibabu na muda wa kumpatia mgonjwa matibabu ili kuepusha madhara zaidi yanayoweza kumpata.



Dalili za ARF
Katika hatua za mwanzo mwanzo, baadhi ya waathirika wanaweza wasioneshe dalili zozote za tatizo hili. Dalili ni kama

    Kupungua kwa uzalishaji mkojo
    Kuvimba mwili
    Kupoteza umakini
    kuchanganyikiwa
    Uchovu
    Kulegea mwili
    Kichefuchefu na kutapika
    Kuharisha
    Maumivu ya tumbo
    Kuhisi ladha ya chuma na uchachu mdomoni
    Na katika hatua za mwisho kabisa, mgonjwa anaweza kupata degedege na hatimaye kupoteza fahamu (coma).



Vipimo na uchunguzi

    Kama ilivyoainishwa hapo juu kuwa baadhi ya wagonjwa wanaweza wasiwe na dalili zozote za tatizo hili. Hata wale wenye kuonesha dalili, zinaweza zisiwe mahsusi (non-specific). Uchunguzi wa mwili unaweza usioneshe tatizo lolote lile, au kukawa na dalili chache sana ambazo zinaweza zisimsaidie sana daktari kufikia uamuzi.
    Baadhi ya vipimo vinavyoweza kugundua uwepo wa ARF ni pamoja na Kipimo cha utendaji kazi wa figo (Renal function tests) ambacho husaidia kuchunguza kiwango cha urea (blood urea nitrogen (BUN) katika damu. Aidha husaidia pia kuchunguza ongezeko la kiwango cha creatinine katika damu.
    Uchunguzi wa kiwango cha madini mbalimbali katika damu (blood electrolytes)
    Uchunguzi wa damu (Full Blood Picture): Husaidia kuonesha uwepo wa maambukizi ya bacteria na/au upungufu wa damu mwilini (anaemia)
    Kupima kiasi cha mkojo kinachotolewa na mgonjwa katika masaa 24
    Uchunguzi wa mkojo (Urine analysis): Rangi ya mkojo, kiasi cha electrolytes, uwepo wa usaha au damu au casts.
    Ultrasound ya figo na kibofu cha mkojo
    Renal biopsy.



Matibabu ya ARF
Matibabu ya ARF hutegemea kwanza chanzo chake na pili ukubwa wa tatizo. Kujua chanzo cha tatizo husaidia kufahamu ni aina gani ya matibabu yanayohitajika wakati kufahamu ukubwa wa tatizo huathiri uchaguzi wa aina ya matibabu na hata hitaji la kufanya dialysis. Hata hivyo inashauriwa sana kumpeleka mgonjwa kwa daktari bingwa wa magonjwa ya figo (nephrologist) kwa matibabu zaidi.

Kulingana na chanzo cha ARF, baadhi ya matibabu yanayoweza kufanyika, hutolewa yakiwa na lengo la:
Kurekebisha kiasi cha upotevu wa maji mwilini ambapo mgonjwa hupewa i.v fluids pamoja kurekebisha kiasi cha madini (electrolytes) kilichopotea
Kupunguza au kuzuia ongezeko la maji kwa wagonjwa ambao figo zao zimeshindwa kabisa kutoa maji nje ya mwili
Kuongeza uwezo wa moyo kufanya kazi vizuri au kuongeza shinikizo la damu husaidia kuongeza mtiririko wa damu kwenda kwenye figo
Kurekebisha kiasi cha madini mwilini kitendo ambacho husaidia mwili kufanya kazi zake vema

Dialysis
Iwapo pamoja na matibabu hayo, figo za mgonjwa zinaendelea kudorora, mgonjwa hana budi kufanyiwa dialysis. Dialysis ni kitendo cha kutoa uchafu na maji yasiyohitajika katika damu. Kitendo hiki hufanywa kwa kupitia mishipa ya damu iliyo chini ya ngozi (hemodialysis) au kwa kupitia tumboni (peritoneal dialysis). Katika hemodialysis mirija hii huunganiswa kwenye mashine ambayo hufanya kazi kama figo. Damu kutoka kwa mgonjwa huingia katika mashine kisha huchujwa ili kuondoa sumu, uchafu pamoja na maji yasiyohitajika kabla ya kurejeshwa tena mwilini.

Kitendo hiki hufanyika angalau mara mbili mpaka tatu kwa wiki, na kwa kiasi fulani ni ghali na si watu wote wa kipato cha chini wanaoweza kumudu gharama zake.

Katika peritoneal dialysis, uchafu pamoja na maji kutoka katika mzunguko wa damu huingia katika nafasi inayotenganisha tumbo na utando wake (peritoneal space), huchujwa kwenye utando huo kisha hutolewa kupitia sindano maalum (catheter ) iliyowekwa juu ya ngozi na kuingia ndani ya tumbo (peritoneal cavity).

Matarajio
Wagonjwa wengi wenye ARF hupona bila hata kuhitaji dialysis mara tu chanzo cha tatizo kinapogundulika na kushughuikiwa mapema. Hata hivyo wakati mwingine, pamoja na matibabu, baadhi ya figo hushindwa kurudia kufanya kazi kwa ufanisi wake wa awali. Watu kama hawa hawa wanahitaji kufuatiliwa kwa ukaribu na umakini mkubwa.

Kinga ya ARF

Inashauriwa

    kufanya uchunguzi wa figo walau mara moja kila mwaka. Hii husaidia kuchunguza utendaji wa figo na hivyo kuepuka madhara kabla hayajatokea.
    Kunywa maji kwa wingi ili kuyafanya mafigo yatende kazi zake kwa ufanisi.
    Kuepuka matumizi ya vitu ama madawa yanayoweza kuathiri nyama, seli au tishu za figo. Ni vema kutumia dawa pale tu unaposhauriwa na daktari.
    Watu wenye hatari ya kupata tatizo sugu la kushindwa kufanya kazi kwa figo (Chronic Renal Failure) wanashauriwa kufanya vipimo na cuhunguzi mara kwa mara
    Muone mtaalamu wa afya mara tu uonapo dalili za kuwepo kwa shida katika kukojoa au uonapo damu katika mkojo.

Wednesday, 3 January 2018

Ujue Mfumo unaosababisha Tatizo la Nguvu za Kiume
 
kwa sasa kuna wimbi kubwa la watu ambao wanasumbuliwa na tatizo la nguvu za kiume, wengi wao matatizo yao yanatumiika kwa kubadili mfumo wa maisha tu na wachache ambao wamejiharibu kwa kujichua na magonjwa mengine ndio wanaweza kuhitaji matibabu ya muda fualani.

katika tafiti zangu nimegundua yafuatayo ni chanzo cha kuishiwa nguvu za kiume, changamoto ambayo imeletwa na mfumo wa maisha.

1. Msongo mkubwa wa mawazo; nguvu za kiume na hamu ya kushiriki tendo hili huanzia kichwani mpaka kwenye uume wa binadamu, watu wenye misongo ya mawazo sababu ya kushindwa kutimiza wajibu wao wa kazi waliopewa kwa wakati, misongo ya mawazo sababu ya majukumu makubwa ya kifamilia ambayo yanakuja na huenda hakuna fedha za kukabiliana na hali hizo, msongo wa mawazo wa biashara zinazoyumba humfanya mwanaume asiweze kushiriki kabisa tendo la ndoa... omba msaada kama kazi zimekuzidi tafuta msaidizi kama umeajiajiri, kama waliokuajiri hawakuelewi tafuta kazi nyingine na uachane na hiyo kazi ya kufanya kazi usiku mpaka usiku lakini pia muda wa kazi ukiisha undoka kwenda nyumbani haraka kwenda nyumbani hakuna sifa ya kufanya kazi masaa mengi wakati mahusiano yako yanakufa.watu wanaofanya kazi benki ni wahanga sana wa matatizo haya.

lakini pia dawa zinazotolewa kutibu msongo wa mawazo huharibu nguvu hizi za kiume pia.

2. Ulevi wa kupindukia; unaweza kua unapenda kunywa pombe angalau kustarehe na kuonana na ndugu na jamaa lakini unywaji wa pombe kupitiliza ni hatari sana, humaliza nguvu za kiume na kukosesha hamu. habari njema ni kwamba pombe kidogo angalau pia moja mpaka mbili kwa siku ni nzuri kwa nguvu za kiume na afya ya moyo.

3. Dawa mbalimbali; baadhi ya dawa zinzotumika kwa shida mbalimbali au magonjwa mbalimbali zimethibitika kupunguza nguvu za kiume hasa zile zinazomezwa mara kwa mara au kila siku mfano dawa za presha, dawa za maumivu na dawa za msongo wa mawazo.

kumbuka usiache dawa kama una ugonjwa unaohitaji dawa kila siku sababu umesoma hapa, kwa upande mwingine uhai unaweza kua muhimu kuliko nguvu za kiume.                                                

4. kufikiria sana; huwezi kupata nguvu za kiume kama unafikiria mambo mengi yanayokuathiri labda maumivu ya vifo ya wapendwa, maumivu ya kuachishwa kazi, maumivu ya kusalitiwa na mpenzi au kuachwa, na uchovu sana wa shughuli za kila siku. jaribu kurelax, kukubali matokeo, kupata usingizi wa kutosha na kushiriki mazoezi na kumbuka mazoezi yakiwa makali sana humaliza nguvu za kiume.    
                      
5. Hasira; hasira juu ya mwenzi wako au mtu yeyote aliyekukwaza hufanya ushindwe kushiriki tendo la ndoa, hakikisha unamwambia mpenzi wako mambo yanayokukwaza...kuyaweka moyoni haitakusaidia hata kidogo.

6. Wasiwasi; wanaume wakishapata matukio kadhaa ya kuadhirika na kushindwa kufanya tendo la ndoa huanza kuogopa kukutana tena na mwanamke kwa hofu kwamba wataadhirika tena...tafuta chanzo ni nini na urekibishe, huenda siku hiyo haukua vizuri au ulikua na njaa...kisha jiamini kwamba sasa ntafanikisha.

7. Vitambi na unene; vijana wengi kwanzia miaka 30 mpaka 40 hilo ndio tatizo lao kubwa, yaani kukosa nidhamu ya kupambana na ungezeko la miili yao na matokeo yake uume hua mdogo na nguvu kidogo sana lakini pia ulaji wa vyakula vya haraka kama chips na mikaango mbalimbali wakati wa kazi na kusahau vyakula asilia kama mihogo,karanga, ugali,wali, matunda na mboga za majani...asikudanganye mtu kama umeshindwa kupungua uzito nguvu za kiume utazisikia redioni.

8. kutojiamini; baadhi ya wanaume hushindwa kujiamini kwa kujikosoa vitu mbalimbali vilivyoko kwenye miili yao ambavyo wakati mwingine hata mwanamke mwenyewe havijali sana mfano kuhisi ana uume mdogo sana wakati uume wake ni wa kawaida, kuhisi hana mwili mzuri na kadhalika.
                                                          
9. Kukosa hamu ya tendo la ndoa; kwa maisha ya sasa hii husababishwa na kuchoka sana na kazi na kukosa muda wa kupumzika, kuna watu wanafanya kazi kila siku ya maisha yao kwa madai wana roho za kichaga...hizo pesa unazotafuta huku unaharibu afya hazitakusaidia kwa lolote hata ukizipata mwisho wa safari na utaibiwa mke na walafi wa mtaani.
                       
10. Magonjwa; haya ni magonjwa mbalimbali ambayo hua hayaponi au huchukua muda sana kupona kwa namna moja au nyingine huharibu nguvu za kiume moja kwa moja mfano kisukari, presha, ajali za migongo na magonjwa ya mishipa ya fahamu, madonda ya tumbo, kifua kikuu, pumu na kadhalika...
                                             
Mwisho; unaweza kua unaona aibu kuongea na daktari kuhusu tatizo lako lakini kimya chako hakitakusaidia, jaribu mwenyewe kufikiri chanzo ni nini ili uweze kubadili mfumo wako wa maisha kama kupunguza uzito, kupunguza kazi na kuishi kwa uwezo wako wa kifedha,kuacha kutumia dawa zinazoharibu nguvu zako, kupunguza ulevi na hata kupata matibabu kama ikionekana ni muhimu

Sunday, 31 December 2017

Wednesday, 27 December 2017

FAHAMU MAMBO YA MSINGI JUU YA HUDUMA YA KWANZA

Tumewapoteza ndugu zetu wengi sana au rafiki zetu au jamaa zetu wengi kwa sababu ya mshtuko(Shock) iliyosababisha kifo chao. Hii ni kwa sababu watu wengi hawajui jinsi ya kumsaidia mtu mwenye mshtuko kabla ya kumpeleka hospitali. Leo nakuletea makala inayokufundisha hatua zote za kufanya ili kumsaidia mtu mwenye mshtuko. Naomba uwe na mimi mpaka mwisho wa makala hii. 

Kwenye somo langu lililopita nilikuelezea jinsi ya kutoa huduma ya kwanza kwa mtu aliyepata ajali na leo naendelea kukufundisha kuhusu namna/jinsi ya kutoa huduma ya kwanza kwa mtu aliyepata mshtuko.

Cha msingi kila mmoja anatakiwa kuwa na vifaa vyote au baadhi vya kufanyia huduma ya kwanza ambazo nilizitaja kwenye makala  iliyopita ili tusaidiane wakati wowote.

Tuanze kwa kujua kuhusu mshtuko.
Damu huzunduka kwenye mwili wa binadamu kutoka kwenye moyo na kusambaa kwenye sehemu zote za mwili kwa kupitia mirija ya damu inayotumika kusafirishia hiyo damu, wakati huu damu inayozunguka mwilini huwa imebeba hewa ya oksijeni kwenye ogani (Organs) na misuli (Tissues) zote za mwili. hii hutokea kwenye hali ya kawaida ya moyo kufanya kazi.

 MSHTUKO ni pale mfumo mzima wa kusafirisha damu mwilini unaposhindwa kufanya kazi vizuri. Hali hii hutokea mara nyingi baada yamtu kupata ajali, maumivu au ugonjwa wa ghafla (sudden illness) hasa hasa kama huu ugonjwa wa ghafla unaambatana namaumivu.
Sababu kubwa sana zinazoweza kusababisha mshtuko ni kuvuja damu kwa wingi inayozidi lita 1.2 kwa muda mfupi, upungufu wa maji mengi mwilini unaosababishwa na kuharisha, kutapika, utumbo kujisokota (intestinal obstruction) na kuungua moto.

Dalili za mtu aliyepata mshtuko;
Mtu mwenye mshtuko anaweza kukosa hewa kwenye akili, dalili zingine za mtu mwenye mshtuko ni;

    Mapigo ya moyo kwenda kwa kasi.
    Mgonjwa kuwa dhaifu.
    Mgonjwa anapauka mwili.
    Mwili kuwa wa baridi na ngozi kukakamaa.
    Kutokwa jasho.
    Anabadirika rangi Cyanosis) hasa kwenye midomo, vidole au kwenye masikio.
    Kizunguzungu.
    Kichefuchefu na hata kutapika.
    Anavuta pumzi kwa shida.
    Kiu.
    Kutokutulia lakini pia anakuwa mkali.
    Kupiga miayo sana.
    Kutokujitambua na mwisho moyo unashindwa kufanyakazi na mgonjwa anaweza kufa.

Baada ya kuzijua dalili za mtu mwenye mshtuko, twende sasa tukajifunze namna ya kumhudumia huyu mgonjwa kwa huduma za dhalula kabla ya kumpeleka hospitali.

JINSI YA KUTOA HUDUMA YA KWANZA KWA MTU MWENYE MSHTUKO.

    Kama unajua chanzo cha mshtuko mfano kuungua au kutokwa damu nyingi, ni bora zaidi ukatibu tatizo ili kupunguza uwezekano wa kuumiza ogani (Organs) za mwili na baada ya hapo uendelee kumpa hudumia kama nilivyokuandikia hapa chini.
    Mlaze mgonjwa chini sehemu ya wazi na yenye hewa safi. hakikisha ulipomlaza siyo pa baridi sana. weka miguu juu kidogo zaidi ya kichwa ili kusaidia damu kuzunguka hadi kwenye akili kichwani.
    mtie moyo mgonjwa mara kwa mara pindi anapoanza kuzinduka.
    Fungua na ulegeze sehemu zote za mwili wake ziliyofungwa na kukazwa kwa nguo zake kama kiunoni, shingoni mikononi n.k.
    Wakati unaendelea WAPIGIE SIMU WATU WENYE GARI LA KUBEBA WAGONJWA (ambulance)
    Mpime mgonjwa vipimo vya kuangalia mapigo ya moyo. (Nitatoa elimu jinsi ya kupima mapigo ya moyo kwenye masomo yajayo)
    Kama mgonjwa hajitambui kabisa. inabidi umfungue kwenye njia ya hewa na umuangalie kama anapumua vizuri. (utamtambua kwa kuangalia kama kifua  kinapanda na kushuka hata kama ni kwa shida) Lakini kama hapumui vizuri tumia kiganja chako kusukuma kidogo kifua chake kuelekea ndani mara kwa mara huku ukiendelea kuangalia kama ameanza kupumua.
    Mshtuko (shock) ni ugonjwa unaotishia maisha ya binadamu kwani unatokea pale hewa safi ya oksijeni inapokosekana kwenye ogani mhimu za mwili kama vile akili, moyo na mapafu, kwa hiyo  mgonjwa anahitaji huduma ya HARAKA SANA anapopatwa na mshtuko ili kuzuia uharibifu au kutokufanya kazi kwa ogani muhimu za mwili.

Mshtuko unaweza kuwa tatizo kubwa sana kama mgonjwa atakuwa na maumivu makali na uoga pia.

Thursday, 21 December 2017

Dondoo Za Afya Leo.


NJIA SITA ZA KUNYWA MAJI YA MOTO ZINAZOTIBU MWILI WAKO.
 
Kunywa kikombe kimoja cha maji ya moto kila asubuhi kinaweza kukutibu mwili wako kwa kusaidia umeng’enywaji wa chakula na kuzuia kuzeeka mapema kabla ya wakati.
Wengi wetu huianza asubuhi vyema kwa kikombe cha kawaha ya moto au chai ya moto kwa lengo la kuuchangamsha miili yetu baada ya kutoka kitandani.

Na pale tunapokunywa maji, basi wengi wetu hupendelea kunywa ya baridi, lakini kwa mujibu wa watalaam wa afya wanatuambia kua tunafanya makosa kufanya hivyo. (kunywa maji baridi)
Mara nyingi unywaji wa maji moto au uvuguvugu, hususani nyakati za asubuhi, inasaidia kuiponya miili yetu na kuitibu pia,
kwa kusaidia kuongeza nguvu katika mmeng’enyo wa chakula ma kupunguza taka mwilini, taka ambazo zinaweza kuzuia kinga zetu kua katika hali yake nzuri ya mfumo sahihi na ambao tunauhitaji.
“matabibu wanasema na kushauri kunywa maji moto ama uvuguvugu nyakati za asubuhi, kila siku, sambamba na mchanyanyo wa maji ya limao, au chai ambayo haina madhara kwa mwili”.
Utumiaji wa maji moto ama vuguvugu huongeza ukazwaji wa utumbo, ambapo husaidia uondoaji wa vitu visivyotakiwa.
Tofauti na maji moto, utumiaji wa maji ya baridi yenyewe huzuia vitu muhimu ikiwemo madini ambayo hua si rafiki kwa mazingira hayo katika mfumo wa umeng’enywaji unapokula chakula.
Kwa wanywaji wa maji ya baridi, inashauriwa kutangulia kunywa maji hayo ya baridi dakika 20 kabla ya kula hata kama maji hayo yanatoka katika vyanzo vya asili vya maji.
Wakati unywaji wa maji ya moto ama vuguvugu yanaweza yasiwe mazuri kwa ladha yanapokua mdomoni,
Hizi hapa zifuatazo ni sababu kwanini tunywe maji ya uvuguvugu,
1. Hurahisisha umeng’enywaji wa chakula,
Maji ya moto ama vuguvugu katika kikombe uamkapo asubuhi yanaweza kuusaidia mwili wako kutoa nje sumu katika mwili.
Maji na vimiminika vingine husaidia kuvunja vunja chakula katika tumbo na kuweka mfumo wa chakula kuwa katika hali nzuri ndani ya mwili. Maji moto au vuguvugu husaidia kuweza kuvunja vunja chakula hicho kwa uharaka zaidi, na hivyo umeng’enywaji wa chakula kua mwepesi na wa haraka.
Unywaji wa maji ya baridi wakati ama baada ya mlo wako unaweza kusababisha kusaidia kugandishwa kwa mafuta ambayo unayapata kupitia chakula, na hivyo kusababisha mrundikano wa mafuta katika utumbo.
Uongezwaji wa barafu ili kutengeneza maji ya baridi hufanya kubadili mfumo halisi wa madini na virutubisho katika mwili ambavyo madini hayo ni muhimu katika kuuweka mfumo wa chakula katika hali ya afya, ambapo pia unaweza kufanya njia mbadala kwa kunywa chupa ya maji ya baridi sambamba na chupa ama glasi ya maji ya uvuguvu au moto ili kusaidia umeng’enywaji wa chakula, hususani baada ya kula chakula chako.
3. husaidia kulainisha choo
Kwa pointi moja au nyingine, wengi wetu tunakabiliwa na vidonda hususani matatizo ya tumbo ambapo hua na choo kidogo au kukosa kabisa haja kubwa.
Vile vile ugumu wa haja uendapo msalani wakati wa kukitoa, husababisha kuchanika au kuchubuka katika sehemu ya kupitia haja kubwa,
Haya yote yanaletwa na ukosefu wa maji mwilini.
Unywaji wa maji moto au vuguvugu nyakati za asubuhi wakati tumbo likiwa halina kitu unaweza kusaidia utumbo mpana kusukuma uchafu/ kinyesi vizyri na kusaidia kuwa na choo laini {kinyesi chepesi} wakati wa uvunjwaji wa chakula na hata usafirishwaji wake hua mzuri kupita utumbo.
Hivyo uchangamshwaji wa utumbo na maji moto husaidia kuurudisha mwili katika ufanyaji wake mzuri na wakawaida wa kazi vyema.
3. huodoa maumivu
Maji ya moto au vuguvugu, tukizingatia ni maji asilia ambayo wengi wetu katika majumba hutumia, husaidia kuondoa maumivu ya tumbo la hedhi kwa wakina mama na maumivu ya kichwa.
Umotomoto toka kwenye maji moto huweza kua na athari chanya katika misuli ya tumbo, ambapo huweza kusaidia kuondoa papo kwa papo makazo na misuli kujinyoosha.
Kwa mujibu wa Healthline, wanasema maji moto au vuguvugu ni mazuri kwa maumivu, ambapo kimiminika hicho cha moto huongeza mzunguko wa damu kwenye ngozi na kusaidia kushusha maumivu ya misuli.
4. Husaidia kupunguza uzito
Kama uko katika mlo wako, unywaji wa maji nyakati za asubuhi basi unaweza kukusaidia katika kupunguza uzito.
Maji moto ama uvuguvugu husaidia kuongeza joto la mwili, ambapo huongeza metabolic/ kiwango cha ufanisi wa kazi katika mwili.
Kadri kiwango cha ufanisi wa kazi katika mwili kinapoongezeka huuruhusu mwili kuchoma kalori nyingi katika mwili.
Hivyo husaidia figo na gastro intestinal kufanya kazi zake vizuri mwilini.
“madaktari wanashauri kua unywaji wa maji moto nyakati za asubuhi, kila siku, pamoja na limao ndani yake, au chai huondoa vitu hatari mwilini”.
Unywaji wa glasi kadhaa za maji moto au vuguvugu na limao ndani yake husaidia kuvunjavuja tisu za mafuta katika mwili na husaidia mmeng’enyo wa chakula.
5. Kuboresha mzunguko wa damu
Mrundikano wa mafuta katika mwili huondolewa wakati wa unywaji wa maji ya moto.
Hii husaidia kuondoa sumu ambazo hua zimezunguka katika miili yetu kwa kufanikisha mzunguko wa damu.
6. Hupunguza hatari ya kuzeeka mapema
Hii inaweza kuzuilika kwa kunywa maji moto ama vuguvugu, upatikanaji wa sumu katika mwili hupelekea kuzeeka mapema na kwa haraka, lakini maji moto ama vuguvugu YAnaweza kusaidia kusafisha mwili kwa kutoa sumu mwilini, hata hivyo pia kuirekebisha ngozi kwa kuoneza SelI mpya maeneo ya ngozi.
Medical Daily linasema kua “wanawake siku zote hunufaika kwa sababu wanakua na homoni nyingi zaidi ambazo huhusika na maji moto,”
Kuweza kua ama kuongeza uimara wa afya yako kupitia unywaji wa maji moto ama vuguvugu, kunywa kila siku asubuhi maji pekee au yaliyochanganywa na limao kwa kuyapa ladha.
Wanywaji wa maji vuguvugu au moto kwa, kadiri wanavyokunywa maji hayo wanaweza kua wanaangamiza tisu za mdomoni na hata maeneo ya koromeo.
Baada ya kuunguzwa na maji hayo ya moto,
Basi huna budi kuyaacha yapoe kidogo kabla ya kuanza kuyatumia kwa kuyanywa.
Vile vile inashauriwa “ kila mara umuone daktari kwa maelezo kabla ya kuanza kunywa maji hayo ya moto, kama utakua katika matumizi mengine ya dawa, ambazo zinaweza kuleta madhara katika ufanisi wa dawa husika