Agizo la Waziri wa Afya kuhusu wagonjwa Muhimbili kuhamishwa na kusitishwa kwa rufaa
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu, ameagiza wagonjwa wasiotakiwa kufanyiwa upasuaji waliopo hospitali ya taifa Muhimbili kuhamishiwa hospitali ya Mloganzila.
Waziri Ummy ametoa agizo leo alipotembelea hospitali ya Chuo cha Afya na Sayansi shirikishi Kampasi ya Mloganzila Jijini Dar es Salaam. Ameeleza lengo kuu la kuhamishwa kwa wagonjwa hao ni kupunguza msongamano katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Ummy ameongeza kuwa Wizara yake imejipanga kuongeza madaktari bingwa kutoka hospitali ya Taifa Muhimbili kwenda kuwahudumia wagonjwa watakao hamishiwa katika hospitali ya Mloganzila.
Pia amezitaka hospitali za Wilaya kama Amana na Mwananyamala kuwapa rufaa wagonjwa wasiohitaji upasuaji ya kwenda Mloganzila.
Kwa Upande wake Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Huduma na Hospitali ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili Kampasi ya Mloganzila, Professa Said Abood, amesema kuwa wamejipanga kuhudumia wagonjwa wote watakao wasili kutoka Muhimbili.
Profesa Abood ametaja Magonjwa yaliyoagizwa kutibiwa hospitalini hapo kuwa ni yale yasiyo hitaji upasuaji kitaalamu yanaitwa Magonjwa ya ndani kama vile Malaria, na mengine. Aidha Abood amesema tayari wameshaanza kuwapokea wagonjwa hao wanaotoka Muhimbili.
0 comments: