Sunday, 14 January 2018

Kijana wa miaka 20 ajishindia $451m kwa bahati nasibu Marekani

Kijana wa miaka 20 mjini Florida nchini Marekani anasema kuwa anapanga kujifurahisha baada ya kutangazwa mshindi wa $451m katika mchezo wa bahati nasibu.

Shane Missler alifananisha nambari tano na mpira wa bonassi ili kujishindia zawadi hiyo ambayo ni ya nne kwa ukubwa katika historia ya mchezo huo nchini Marekani.

Alitarajiwa kulipwa malipo ya kwanza ya $282 badala ya fedha zote kwa kipindi cha mda mrefu.

Bwana Missler alisema alikuwa na hisia kwamba ataibuka mshindi mkesha wa usiku wa droo hiyo ya mamilioni ya dola.

Dakika chache baadaye droo hiyo wiki moja iliopita alichapisha ujumbe katika mtandao wake wa facebook: Oh My God.
Bwana Missler aliwasilisha tiketi yake ya ushindi katika makao makuu ya mchezo huo wa bahati nasibu katika eneo la Tallahassee siku ya Ijumaa akiandaman na babake na wakili.

Amesema kuwa ana mipango mikubwa na fedha hizo.Nina miaka 20 pekee.

''Lakini natumai kutumia kufuatilia mambo yangu ya kibinafsi niliotaka kufanya, kusaidia familia yangu mbali na kusaidia jamii'', alisema bwan Missler kulingana na taairfa hiyo.

0 comments: