Thursday, 11 January 2018

UNHCR kulaani mpango wa Israel juu ya wahamiaji kutoka Afrika


 
Umoja wa Mataifa umelaani mpango wa Israel wa kuwaondoa wakimbizi kama usioeleweka na si salama, unaokusudia kuwafukuza maelefu ya wakimbizi Waafrika nchini humo.

Shabaha ya mpango wa Israeli inawahusu wakimbizi 38,000, wengi wao ni Waeritrea na Wasudan. Yasemwa akufukuzaye hakuambii ondoka, muondoko huo umepakawa sukari ya $3,500 na tiketi ya ndege kwa kila mkimbizi. Wakimbizi hao wakikataa, kufikia Machi mwaka huu 2018, watakamatwa.

Shirika la wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR liliukosoa vikali mpango huo na kutoa wito kwa Israel isimamishe sera hiyo, kwa sababu haieleweki wala haitekelezwi kwa njia wazi.

Mpaka sasa Israeli haijasema wapi wakimbizi hao wanakwenda. Lakini kwa mujibu wa watetezi nchini Israeli, kuna mapatano baina ya Israel na Uganda na Rwanda kuwapokea wakimbizi hao ilimradi wameridhia. 
Ingawa Uganda na Rwanda mara kadhaa zimekanusha kuwepo kwa maafikiano aina hiyo. Watu 80 ambao walihojiwa Roma na UNHCR, walisema walipelekwa kwa ndege hadi Rwanda na $3,500 kila mmoja. Licha ya kuwa waliondoka Rwanda. wakaelekea kaskazini kupitia maeneo ya vita Sudan Kusini, Sudan na Libya, na kuhatarisha maisha kuvuka Bahari Mediterranean kuingia Italia huku njiani waliteswa na kunyanyaswa.

0 comments: