Sunday 14 January 2018

AZAM SC MABINGWA MAPINDUZI CUP

Ubingwa wa Mapinduzi Cup 2018 ilioutwaa klabu ya Azam, unaifanya klabu hiyo ya Tanzania bara kuandika historia mpya katika mashindano hayo baada ya kuifunga URA kwa penati 4-3 kwenye mchezo wa fainali ulioshuhudia dakika 90 zikikatika huku timu hizo zikiwa hazijafungana.
Azam imekuwa klabu ya kwanza kubeba kombe la mapinduzi mara nyingi kuliko vilabu vyote vilivyowahi kushiriki mashindano hayo tangu yalipoanzishwamiaka 11 iliyopita. Ubingwa wa mapinduzi 2018 ni wa nne kwa Azam ambao waliwahi kutwaa taji hilo katika miaka ya 2012, 2013 na 2017.
Azam wameirudia rekodi yao ya kutetea ubingwa wa Mapinduzi waliyoiweka mwaka 2012 na 2013, mwaka 2012 ndiyo ilikuwa mara ya kwanza kwa klabu hiyo iliyoanzishwa mwaka 2007 kushinda kombe hilo ambalo walilitetea tena mwaka 2013. Mwaka 2017 walishinda ubingwa huo kwa mara ya tatu kisha kuutetea tena mwaka huu 2018.


0 comments: