Sunday 7 January 2018

Kingwangalla awaonya wanasiasa Kilombero



Waziri wa Maliasili na utalii Dkt Khamisi Kigwangalla amesema hatowafumbia macho wala kuwaonea haya baadhi ya wanasiasa wanaounga mkono wananchi kuvamia bonde la mto Kilombero na kufanya shughuli za kilimo na ufugaji kwani bonde hilo ni tegemeo kwa uhifadhi wa wanyama pori pamoja na maji yake kutumika katika uendeshaji wa mtambo wa kufua umeme unao jengwa.

Waziri Kigwangalla ameyesema hayo wilayani Kilombero katika ziara yake kutembelea mipaka ya wanakijiji na hifadhi ya bonde hilo na vijiji vya kata ya Namawala akiwa ameambatana Naibu waziri wake Japhet Hasunga na viongozi mbalimbali wa chama na serikali ambapo amesema hayupo tayari kuwavumilia baadhi ya wanasiasa wanaokwamisha malengo ya serikali kwa makusudi.

Kwaupande wao wananchi waliovamia katika hifadhi hiyo wamemuomba waziri mwenye dhamana kuona namna ya kuwasaidia kuharakishwa kwa mipaka ili wananchi hao waendelee na shughuli za maendeleo.

Hata hivyo baada ya mkutano na wananchi Waziri akiwa na Naibu wake walitembelea mipaka ya wanakijiji na hifadhi ya bonde hilo ambapo alilazimika kuwa mbogo baada ya kutoridhishwa na utenda

0 comments: