Friday, 12 January 2018

Makanisa ya kuchonga kuijenga Yerusalemu mpya bado yapo Ethiopia

Lalibela katika Ethiopia ya Kaskazini ni nyumba ya makanisa ya kale na ya kuvutia ambayo yalifunikwa mwishoni mwa karne ya 12.

Makanisa hayo yaliagizwa na mfalme Lalibela ambaye alitaka kujenga Yerusalemu mpya kwa wasomi wake.

Wanahistoria wengi waliamini kwamba sanaa ya kuchonga makanisa ilikwisha zaidi ya miaka 500 iliyopita. Lakini hata leo, uvumbuzi mpya wa makanisa hayo unaendelea.

Prof Michael Gervers ni mhadhiri wa Historia katika Chuo kikuu cha Toronto nchini Canada na amekuwa akifanya utafiti wa makanisa yaliyochongwa kutoka kwa mawe kwa zaidi ya miaka thelathini.

Na anasema watafiti wengi wanakubali kwamba taaluma hii ya kujenga makanisa ya miamba ilikiwisha mwishoni mwa karne ya 15.

Lakini kama tulivyopita zaidi ya miaka mitatu iliyopita, hili ni jambo linaloendelea.
Wakati Gebremeskel Melegeta ambaye anasimamia ujenzi huo amethibitishia kwa ulimwengu kuwa makanisa ya Lalibela yalijengwa na raia wa Ethiopia.

"Haya ni mapenzi ya Mungu, kazi ya Roho Mtakatifu. Hatujawahi kuona mipango yoyote au ramani yoyote ya miundo hii. Tulianza kazi yetu na Roho Mtakatifu alituongoza na unaweza kuona matokeo ni haya."

Baadhi ya mifano bora ya usanifu wa makanisa ya mwamba iliyochongwa kutoka mwamba mmoja hupatikana katika mji wa Laibella Kaskazini mwa nchi.

Makanisa kumi na moja ya monolithic, kama yanavyoitwa, yaliagizwa na Mfalme Lalibela mwishoni mwa karne ya 12.

Kwa muda mrefu wataalamu wameamini kwamba ufundi huo ulipotea miaka 500 iliyopita lakini kuna uwezekano mzuri sana kwamba wakati nguvu zaidi za umeme zitapatikana nchini Ethiopia - ikiwa wanaendelea kufanya makanisa ya miamba - watatumia mashine za kisasa na huenda sasa taaluma hii ikatoweka kabisa.

Makanisa huko Lalibela huchukuliwa kuwa ni maeneo ya safari na hija na hata yametambuliwa na na Umoja wa Mataifa kama maeneo ya Urithi wa Dunia.

Kwa kufufua ufundi huu wa kale ya makanisa yaliyopigwa kwa mkono, kona hii ya Ethiopia inajenga sura mpya katika historia yake.

0 comments: