Saturday 13 January 2018

TANESCO Yatoa Siku Nne (4) Kwa Wadaiwa Sugu Wa Bili Za Umeme Wawe Wamelipa, Vinginevyo Huduma Zinasitishwa


Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) tunautaarifu Umma na Wateja wetu wote kuwa, tumetoa muda wa siku nne (4) kuanzia Januari 12, 2018 hadi siku ya Jumatatu Januari 15, 2018 kwa wadaiwa sugu wawe wamelipa madeni yao.


Baada ya muda huo kuisha Shirika litasitisha Huduma ya umeme dhidi ya Wateja watakaoshindwa kulipa madeni ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua zingine za kisheria.


Ofisi za TANESCO zitakuwa wazi siku ya Jumamosi Saa 3:00 Asubuhi hadi Saa 9:00 Mchana.


mawasiliano
Kituo cha miito ya simu Makao Makuu +255 222 194 400 na +255 768 985 100
Tovuti: www.tanesco.co.tz, mitandao ya kijamii:

Mitandao ya kijamii
Twitter, www.twitter.com/tanescoyetu,
Facebook https://www.facebook.com/tanescoyetultd/

IMETOLEWA NA:
OFISI YA UHUSIANO
TANESCO MAKAO MAKUU

0 comments: