Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Rais wa Zanzibar, Dkt Ali Mohamed Shein, ametoa msamaha kwa wafungwa 12 ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Rais Dkt Shein ametoa msahama kwa wafungwa hao ambao walikuwa wamehukumiwa kwa makosa mbalimbali.
Msamaha huo umetolewa kwa mujibu wa ibara ya 59 ya Katiba ya Zanzibari ya mwaka 1984 ambayo imempa Rais mamlaka ya kutoa msamaha kwa wafungwa.
Msamaha huo unatolewa kwa wafungwa kama nafasi ya wao kuanza kuishi maisha mapya na kuachana na vitendo vya kihalifu.
Wafungwa waliopewa msamaha huo ni;
Abdul-Aziz Abdalla
Omar Abdalla Nuhu
Ali Khamis Mrau
Mussa Ali Vuai
Hassan Seif Khamis
Nassor Abeid Issa
Jihadi Jalala Jihadi
Edward Jemeria Magaja
Sleiman Abdalla Amir
Mtumwa Khamis
Said Seif Omar
Masoud Seif Nassor
Katika hatua nyingine, raia wengi 74 wa Zanzibar (baadhi yao wamefariki) wametunukiwa medali na Rais Dkt Shein kutokana na mchango wao mkubwa katika mapinduzi na pia kuleta maendeleo katika visiwa hivyo.
Miongoni mwao, raia 43 wamepewe medali za mapinduzi huku wengine 31 wakipewa medali za mfano kwa utumishi wao uliotukuta kwa wananchi.
0 comments: