Saturday 13 January 2018

Jalada la Kesi ya Malinzi larudi TAKUKURU

Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) amewarejeshea TAKUKURU jalada la kesi ya utakatishaji wa fedha inayomkabili aliyekuwa rais wa (TFF), Jamal Malinzi na wenzake ili warekebishe vitu vichache vya kiuchunguzi.

Mbali ya Malinzi, wengine ni Katibu wa TFF, Mwesigwa Selestine na Mhasibu wa shirikisho hilo, Msiande Mwanga.

Hayo yameelezwa jana na Wakili wa TAKUKURU, Leornad Swai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri, wakati shauri hilo lilipoitishwa kwa ajili ya kutajwa.

Swai amedai jalada la kesi hiyo limesharudi TAKUKURU likitokea kwa DPP, hivyo wamepewa maelekezo ya kukamilisha baadhi ya uchunguzi.

Baada ya kueleza hayo, wakili wa Utetezi Nehemia Nkonko aliomba upelelezi wa shauri hilo ukamilike kwa haraka kwa sababu washtakiwa wapo ndani.

Hakimu Mashauri ameahirisha kesi hiyo hadi January 25, 2018 kwa ajili ya kutajwa.

0 comments: