Friday 12 January 2018

SAMATTA AJIFUA KWA MAZOEZI MAKALI UBELGIJI

Nahodha wa Tanzania, Mbwana Samatta amerejea uwanjani akijifua na zaidi anapiga tizi kwa juhudi kubwa kurejea katika hali ya ufiti hasa.

Samatta amekuwa akijifua kikosi cha KRC Genk cha Ubelgiji katika mazoezi mbalimbali yakiwemo yale ya majini.
Wachezaji wa Genk wamekuwa wakijifua vilivyo na Samatta ameungana nao baada ya kukaa nje kwa takribani miezi miwili baada ya kuumia goti.


0 comments: