Jeshi la Polisi mkoani Mwanza linawashikilia watu sita akiwemo Ofisa Ardhi wa Manispaa ya Ilemela, Alex Nyabange (30), kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo utapeli wa viwanja, kutengeneza vyeti bandia vya kitaaluma pamoja namba za mlipa kodi za (TIN), za Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA).
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo Alhamisi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amesema watu hao walikamatwa kwa nyakati tofauti kati ya Desemba 30, 2017 na Janauari 9 mwaka huu.
Msangi aliwataja waliokamatwa kwa tuhuma za kuwatapeli watu kwa madai ya kuwauzia viwanja kuwa ni Aloyce Nyabange (30) ambaye ni ofisa Ardhi wa Manispaa ya Ilemela, Alex Josephat(41) ambaye ni mfanyabishara, Juma Malulu (60) mkazi wa mta wa Ilemela.
Wengini ni Katibu Mhatasi wa kampuni ya Nyambale Civil Works, Getruda Peter (42) mkazi wa Nyegezi na mchora ramani Deodatus Bety (51) mkazi wa Usagara ambao wote walikamatwa Desemba 30, 2017 kwa nyakati tofauti.
“Tulipata taarifa hizi baada ya mtu mmoja ajulikanaye kwa jina la Barnabasi Ibengo (39) mfanyabishara wa Kiseke kuwa ametapeliwa na watu waliosema wana viwanja viwili eneo la Nyasaka na kwamba vinahitaji Sh45 milioni, lakini akawa ametanguliza Sh10 milioni akiamini kuwa ni ukweli kutokana na nyaraka zote walizomuonyesha,” amesema Msangi.
Hata hivyo Msagi amesema mfanyabishara huyo, aligundua kuwa ametapeliwa baada ya kwenda eneo vilipo viwanja hivyo na kuonana na mwenyekiti wa mtaa huo na kuaambiwa hakuna jambo la namna hiyo ndipo alitoa taarifa polisi na kuanza kufuatilia kukamatwa mmoja baada ya mwingine.
Alisema watuhumiwa hao walikutwa na komputa inayotumika kutengenezea nyaraka mbalimbali na baadhi ya nyaraka zinazoonyesha viwanja kwa ajili ya kuuzwa.
Kuhusu vyeti feki Kamanda Msangi amesema walimkamata Evancy Wilson (33) katika mtaa wa Buzuruga Ilemela akiwa na vifaa vya kughushi vyeti vya taaluma mbalimbali.
Amesema tukio hilo lilitokea Janauri 9, mwaka huu saa 11:00 jioni ambapo mtuhumiwa baada ya kukamatwa na kuchunguzwa kwenye kompyuta yake walikuta namba inayofanana na TIN ya TRA na vyeti hivyo vya taaluma vya kughushi.
Amesema walikuta vyeti vya kughushi vya, stashahada, shahada, vyeti, vitambulisho vya mpigakura, nyaraka zinazoonyesha kuwa ni za kuombea mikopo benki, leseni za biashara na flash ambazo zimejazwa vitu hivyo.
“Hili lilitokana na taarifa tulizopata kutoka kwa raia wema kuhusu kuwapo kwa mtu anayetenegeza vitu hivyo ndipo tulianza kufuataili, watuhumiwa wote wapo polisi, upelelezi ukikamilika tutawafakisha mahakamani.
0 comments: