Nyota wa tenisi Serena Williams atarejea uwanjani huko Abu Dhabi wiki ijayo miezi minne baada ya kujifungua.
Serena mwenye umri wa miaka 36, atakutana mchezaji nambari saba duniani
Jelena Ostapenko tarehe 30 Disemba wakati wa mechi ya ubingwa wa dunia
ya Mubadala, Alijifungua mtoto msichana Alexis Olympia Ohanian mwezi
Septemba.
Bingwa huyo wa zamani duniani hajacheza tangu alisema Australian Open mwezi Januari.
Mkurugenzi wa Australian Open, Craig Tilley amesema kuwa Williama
anatarajiwa kutetea taji lake katika mechi ya mwaka 2018 ambayo itaanza
Januari 15.
Rafael Nadal, Milos Raonic na Stan Wawrinka wamejiondoa kutoka kwa Mubadala ambayo itachezwa kati ya 28-30 Disemba.
0 comments: