Monday 18 December 2017

UCHAGUZI HONDURAS Rais mpya alochaguliwa ni HERNANDEZ.

Tume ya uchaguzi nchini Honduras imemtangaza kiongozi aliyepo Juan Orlando Hernandez, mshindi wa uchaguzi wa mwezi jana wa urais, licha ya maandamano ya wiki kadhaa kutoka upinzani wanaolalamika kuwepo udanganyifu.
Hernandez amemshinda mtangazaji mashuhuri wa televisheni, Salvador Nasralla, kwa asilimia chini ya mbili.
Upinzani umewaomba raia wamiminike barabarani kupinga uamuzi huo. (BBC SWAHILI)

1 comment: