Israel ilichukua udhibiti wa sehemu ya mashariki mwa mji huo katika vita vya mashariki ya kati mwaka 1967 na inaliona eneo lote la mji wa Jerusalem kuwa mji ambao haukugawanyika.
Wapalestina wanaliona eneo la mashariki mwa Jerusalem kuwa mji mkuu wao wa hapo baadaye.
Balozi wa Israel katika Umoja wa mataifa Danny Danon "anashutumu vikali" mswada huo , akipuuzia kwamba ni juhudi za Wapalestina "kuandika upya historia."
"Hakuna kura ama mjadala utakaobadilisha hali halisi kwamba Jerusalem ilikuwa ama itakuwa mji mkuu wa Israel," danon alisema katika taarifa.
Mswada huo wa azimio unatoa wito kwa nchi zote kujizuwia kufungua balozi zao mjini Jerusalem, ukiakisi wasi wasi kwamba serikali nyingine zinaweza kufuata kile Marekani ilichofanya.
Mswada huo unataka kwamba mataifa yote wanachama kutotambua hatua yoyote ambayo itakwenda kinyume na maazimio ya Umoja wa Mataifa kuhusu hadhi ya mji huo.
Maazimio kadhaa ya Umoja wa mataifa yanaitaka Israel kujiondoa kutoka katika ardhi iliyokamata wakati wa vita vya mwaka 1967 na kusisitiza haja ya kufikisha mwisho kulikalia eneo la Wapalestina. (DW SWAHILI)
0 comments: