Waziri
wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako amewataka wote
wanaodaiwa mikopo ya Elimu ya Juu kuirejesha mikopo hiyo mara moja
pasipo kungoja kuchukuliwa hatua za kisheria.
Katika
mahojiano aliyoyafanya na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), Waziri
Ndalichako alisema kuwa kila aliyepata mkopo wa Elimu ya Juu ana wajibu
wa kuulipa ili wanafunzi wanaoomba mikopo nao waweze kupata na kwamba
serikali haitosita kuchukua hatua stahiki kwa wale ambao hawatozirejesha
ikiwamo kushtakiwa mahakamani.
Waziri
Ndalichako alisema kwa wale waliokuwa wakinufaika na mikopo hiyo na kwa
sasa wamejiajiri wenyewe na ambao bado hawajapata ajira wanapaswa
kufika katika Ofisi za Bodi ya Mikopo ili wapewe utaratibu wa namna gani
ya kuanza kurejesha.
Hata
hivyo Prof. Ndalichako alisema kwamba, idadi ya wanufaika wa mikopo
waliojitokeza kwa hiari kuanza kurejesha mikopo yao imeongezeka na
kuwataka ambao bado hawajaanza kufanya hivyo wawaige wenzao walioanza
tayari.
Novemba
2016, Bodi ya Mikopo ilitoa orodha ya majina ya wadaiwa sugu takribani
20,000 ambao walitakiwa kuanza kurejesha mikopo yao ndani ya siku 30.
Hapo
awali Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu,
Abdulrazaq Badru alieleza kuwa watachapisha orodha ya majina ya wadaiwa
sugu takribani 142,470, wanaodaiwa jumla ya kiasi cha shilingi za
kitanzania 239.3 billioni.
Hata
hivyo Prof Ndalichako aliwataka wale wote watakaoanza kurejesha mikopo
yao kwa Bodi ya Mikopo, kulipa fedha hizo kupitia akaunti ya benki ya
Bodi na siyo kulipa fedha taslimu kwa mtu yeyote yule. Alisisitiza hilo
ili kuepusha usumbufu ikiwemo utapeli ambao unaweza kufanyika wakati wa
ufanyaji wa malipo hayo.
0 comments: