Thursday, 21 December 2017

Wahamiaji wa Nigeria wasimulia visa vya kutisha

Wahamiaji waliorudishwa Libya kutoka Nigeria watakwambia wamesikia visa vya kutisha vinavyowakumba safarini wanapoelekea barani Ulaya kama vile utumwa nchini Libya, kuzama kwenye bahari ya Mediterranean kabla hata kuihama nchi yao kujitafutia maisha bora.
Wanaharakati pia wanasema huwaonyesha video kwenye shule, masoko na hata sehemu nyingine za umma kila mara , kuwahamasisha kuhusiana na maeneo mabaya na hatari ambayo mtu anakumbana nayo kama kutekwa nyara na kupelekwa Ulaya.
Lakini hata habari hizo haziwezi kuwazuia wahamiaji waliojitolea.
Wahamiaji wengi hudhani hao hawatakumbana na bahati hiyo mbaya, amesema Josiah Emerole, kiongozi wa mawasiliano katika shirika la kupambana na ufasirishaji wa binadamu kinyume cha sheria nchini Nigeria.
Tabia hizo zimeanza kudhihirika enzi za mfumo wa Mila na tamaduni nchini Nigeria.


Kabla Ukristo na Uislamu kuwa Imani kuu nchini humo, raia wa Nigeria kama waafrika wengi waliamini kuwa kuna nguvu za giza ambazo zinaweza kudhibiti bahati ya mtu maishani.
Maelfu ya wahamiaji huvuka kuelekea Ulaya kila mwaka na hutuma fedha kwa familia zao kwa matumizi ya ujenzi nyumba na karo kwa ndugu zao kuendeleza masomo yao.
(BBC SWAHILI)

0 comments: