Wednesday 27 December 2017

Kibano cha Maadili kwa Watumishi wa Umma Chaja

Serikali kupitia sekretalieti ya Maadili imewataka viongozi wote wa umma kujaza fomu ya Tamko la Maandishi ambalo linaorodhesha Mali,ama Rasilimali wanazomiliki kabla ya Tarehe 31 Desemba mwaka huu.

Rasilimali hizo ni zile zinazo jumuisha Mali za mke/mume pamoja na watoto wao ambao wamezidi umri kuanzia miaka 18 kuwasilisha kwa Kamishna wa Maadili ,ambapo kwenye tamko hilo litajumuisha mali na rasilimali za kiongozi husika.

Kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania Ibara ya 132 ya 1977 sekretalieti hiyo ya maadili ya viongozi wa umma ni idara inayojitegemea chini ya ofisi ya Rais ,ambayo ilianzishwa kwaajili ya kusimamia utekelezaji wa sheria ya maadili ya viongozi wa umma namba 13 ya mwaka 1995.

Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es salaam leo Kamishna wa Maadili Jaji Mstaafu Harold R. Nsekela amesema sekretalieti hiyo inatoa wito kwa viongozi wa Umma ambao hadi sasa bado hawajapata fomu ,wapitie Tovuti ya www.ethicssecretariat.go.tz ambapo huko ndipo zinapopatikana fomu za Tamko la Rasilimali na Madeni.

Aidha amesema Baada ya kujaza fomu hizo kiongozi atatakiwa kuziwasilisha katika ofisi za sekretalieti ya maadili ya viongozi wa Umma Dar es salaam au katika ofisi kanda ya kati Dodoma,kanda ya ziwa Mwanza,na kanda ya nyanda za juu kusini zilizoko Mjini Mbeya.

Hata hivyo viongozi wamekumbushwa kuwa, ni kosa kwa Mujibu wa kifungu cha 15 (C)cha Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa kiongozi kushindwa kutoa Tamko bila sababu ya Msingi .

Kwa upande wake Afisa Sheria Mkuu wa Sekretalieti ya Maadili ya viongozi wa Umma Bw. Filotheus Manuca amesema kwa mwaka jana hakukuwa na kiongozi yeyote ambae alifikishwa kwenye baraza la Maadili ,na kusema kazi kubwa sekretalieti hiyo ni kuhakikisha kila kiongozi wa Umma anakuwa Muadilifu.

0 comments: