Taarifa zinasema Eboue anataka kufanga jaribio la kujiua kutokana na hali mbaya inayomkabili katika maisha yake, ripoti zinasema kiungo huyo ameyumba sana kiuchumi kiasi cha kuona uhai hauna thamani tena kwake.
Eboue alikuwa akipokea kiasi kikubwa katika klabu ya Arsenal huku akipokea zaidi ya £1.5m wakati akiichezea klabu ya Galatasaray lakini inasemekana kwamba talaka na mkewe huenda ikakomba kila kitu alichonacho.
Eboue na mkewe aliyetambulika kwa jina la Aurellie imemfanya Eboue kuwa na msongo wa mawazo mkubwa unaochangiwa na kuzuiliwa kuwatembelea watoto wake watatu Mathis, Clara na Maeva katika msimu huu wa Xmass.
Inafahamika kwamba Eboue alimpa mamlaka na haki ya kumiliki mali zote walizokuwa nazo na kitendo ya kutalakiana kinamaanisha Eboue atapoteza kila kitu alichomuandikishia mwanamke huyo baada ya kushindwa kesi ya talaka mahakamani.
Achana na majanga hayo ya Eboue lakini mchezaji huyo alitoka kufiwa na babu yake nchini Ivory Coast aliyefariki kwa kansa huku kaka yake aliyefahamika kwa jina la N’Dri Serge naye alifariki kwa ajali ya pikipiki.
Matatizo ya Eboue ya umiliki wa baadhi ya vitu ikiwemo nyumba yake ya kisasa iliyoko London na hana pesa ya kuwalipa watetezi wa kisheria hali ambayo inakaribia kupelekea baadhi ya nyumba na mali alizobakiwa nazo kuuzwa.
“Naogopa hata watu kufahamu kwamba niko ndani, sina amani nikiwa ndani maana nawaza muda wowote polisi wanaweza kuja kuniondoa, siwashi hata taa maana sitaki watu nje wajue kwamba nipo” alisema Eboue.
Eboue analala katika nyumba ya rafiki yake ambapo inasemekana analala chini huku hana hata pesa ya kupelekea nguo dry cleaner hali inayompelekea kutumia mikono yake kufua nguo.
Eboue anasikitisha sana na amesema anatamani klabu yake ya zamani ya Arsenal imsaidie katika kipindi hiki kigumu lakini atajisikia vibaya kama akionana na wachezaji wenzake wa zamani akiwemo Thiery Henry.
Pamoja na yote na pia ni somo kwa vijana wa Kiafrika lakini Emmanuel Eboue haachi kumshukuru Mungu na amesema yote yanayoendelea katika maisha yake ni mpango wa mungu na hatamani yamtokee mtu mwingine.
0 comments: