Vinara wa ligi kuu soka Tanzania bara Simba SC na Azam FC zinajipanga vyema kuhakikisha zinaendelea kuongoza ligi kuu hadi mwaka 2017 unamalizika, ambapo ligi itakuwa imechezwa kwa jumla ya raundi 12.
Simba ambao ni vinara wakiwa na alama 23, kikosi chao kinaendelea na mazoezi kujilinda na mchezo wake wa jumamosi hii dhidi ya Ndanda FC utakaopigwa kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.
Kwa upande wa Azam FC ambao wanashika nafasi ya pili wakiwa na alama 23 sawa na Simba SC, zikitofautina kwa idadi ya mabao ya kufunga na kufungwa inajipanga kuhakikisha inachukua alama zote tatu kwenye mchezo dhidi ya Stand United Ijumaa hii.
Baada ya mazoezi ya jana kwenye viwanja vya Polisi Kurasini kikosi cha Simba kimeingia rasmi kambini na kitasafiri kwenda Mtwara siku yoyote kuanzia kesho. Wakati huo kikosi cha Azam FC kimeendelea na kambi yake kwenye uwanja wa Azam Complex.
Simba ambayo imetoka kumfukuza kocha wake Joseph Omog kutokana na matokeo mabaya kwenye kombe la shirikisho ambapo iliondolewa na Green Worrios, itawekeza nguvu zaidi kwenye ligi ili kutwaa ubingwa na kupata nafasi ya kushirkiki michuano ya kimataifa mwakani.
0 comments: